January 30, 2013

Ngara, majirani zetu Biharamulo wameamua Hivi, sisi je?




Pichani aliyesimama ni mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Biharamulo Bw. Nassib Mmbaga, aliyekaa ni Afisa Mipango wa halmashauri hiyo Bw. Zabron Njanga  wakati wa Kikao cha Baraza la Madiwani kupitisha Bajeti kwa mwaka wa fedha 2013/14 klatika ukum bi wa Halmashauri hiyo

HALMASHAURI YA WILAYA BIHARAMULO KUTUMIA  SHILINGI BILIONI
19,314,305,400 KWA MWAKA WA FEDHA 2013/14.

Halmashauri ya wilaya ya Biharamulo Mkoani kagera imekisia kutumia zaidi ya shilingi bilioni  19.3 katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo  ambazo zitatokana na wahisani mbali mbali,ruzuku ya serikali na vyanzo ya  ndani  ya halmashauri hiyo kwa kipindi  cha mwaka wa fedha  wa 2013 na  2014
Akisoma  mapendekezo  ya bajeti  kwa mwaka 2013/14mweka hazina wa halmashauri hiyo Bw. Alexandar Bashaura amesema kuwa   katika bajeti hiyo kiasi cha shilingi bilioni  4 zinatarajia kutumika katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Bw. Bashaura amesema kuwa kiasi cha shilingi bilioni 10.9 ambazo ni sawa na asilimia 57 zitatumika katika kulipia mishaharara na bilioni  3 .4 zitatumika kwa matumizi mengineyo
Hata hivyo makisio hayo ya bajeti kwa mwaka wa fedha 2013/14 ina ongezeko la shilingi bilioni  3, milioni 143, na laki 7 na 37 elfu sawa asilimia 20 ikilinganishwa na bajeti ya 2012/13 ambapo makisio yalikuwa shilingi Bilioni 16,milioni 170, laki 5 na sitini na 7 elfu.

No comments:

Post a Comment