April 14, 2017

Hospitali Teule ya Sengerema yapewa Msaada

Mganga mkuu wa Hospitali teule wilaya ya Sengerema Sr.Marie Jose akipokea Msaada kutoka kwa Robert Kaseko Mjumbe wa Baraza kuu la umoja wa Vijana wa CCM mkoa wa Arusha 
Watoto 42  wenye umri wa chini ya miaka mitano wamelazwa katika
Hospitali Tuele ya wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza kwa tatizo la kukosa Lishe kati ya januari hadi machi mwaka huu na wawili kati yao kufariki  dunia

Hali hiyo imelazimu Hospitali hiyo kutumia zaidi ya shiingi  Laki sita kila mwezi kugharimia Lishe kwa watoto wanaotambuliwa na kulazwa Hospitalini hapo kutokana na wazazi walio wengi kutofahamu kuandaa Lishe na changamoto ya kipato

Hali hiyo imebainishwa na Sista  Marie Jose mganga mfawidhi wa Hospitali hiyo wakati akizungumza na www.ngarakwetu.blogspot.com baada ya kupokea msaada wa Chakula yakiwemo mahindi,maharage,Sukari,mafuta ya kupikia na Sabuni kutoka kwa Robert Kaseko Mjumbe wa Baraza kuu la umoja wa Vijana wa CCM mkoa wa Arusha ambaye ni mzaliwa wa Wilaya ya Sengerema

Akizungumzia hali ya watoto hao, mratibu wa Lishe wilaya ya Sengerema Bi.Rachel Ntogwisangu  amesema changamoto zinazowakabili wananchi ni pamoja na uelewa mdogo wa maandalizi ya Lishe kwa watoto,Uduni wa maisha na wasishana wadogo wanaozalishwa katika umri mdogo.      
www.ngarakwetu.blogspot.com

No comments:

Post a Comment