September 22, 2012
Meja Jenerali Ndomba Amrithi Gen. Shimbo JWTZ
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa
Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Meja Jenerali Samuel Albert Ndomba
(pichani) kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Aidha, Rais Kikwete amempandisha cheo Meja Jenerali Ndomba kuwa Luteni
Jenerali.
Taarifa iliyotolewa jana, Ijumaa,
Septemba 21, 2012, mjini Dar Es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi
Ombeni Y. Sefue kupitia Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais – Ikulu,
imesema kuwa uteuzi huo unaanza leo.
Taarifa hiyo ya Balozi Sefue imesema kuwa kabla ya uteuzi wake, Meja
Jenerali Ndomba alikuwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
Jenerali Ndomba anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Luteni Jenerali
Abdulrahman A. Shimbo ambaye amestaafu Jeshi kwa mujibu wa sheria baada
ya kufikisha umri wa miaka 60.
Taarifa ya Balozi Sefue pia imesema kuwa Rais Kikwete amemteua Brigedia
Jenerali Raphael Mugoya Muhuga kuwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa
kuanzia jana, Ijumaa, Septemba 21, 2012.
Aidha, Rais Kikwete amempandisha cheo Brigedia Jenerali Muhuga kuwa Meja Jenerali.
Kabla ya uteuzi wake, Brigedia Jenerali Muhuga alikuwa Mkuu wa Utawala na Mafunzo wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment