WANANCHI
WAWACHAPA VIBOKO WALIMU
GEITA
Walimu wawili wa
shule ya Msingi Isabilo iliyopo kata ya
Bugurula wilaya Geita wamevamiwa na
kupigwa kwa fimbo na wananchi waliovamia shule hapo kulipiza kisasi baada ya
walimu hao kuwaadhibu kwa viboko wanamfunzi na mmoja wao kupandisha mapepo
Tukio hilo limetokea Januari 25 mwaka huu hali iliyopelekea walimu
10 wa shule hiyo kugoma kuingia madarasani kufundisha wakiomba serikali
iwahamishe kutoka shuleni hapo kwa madai ya kudhalilishwa na wananchi
Kaimu mkuu wa shule
hiyo mwalimu Athuman Augustine amewataja waliopigwa kuwa ni Mwl. Medan Zacharia na Deograss
Liston
Akizungumzia na
tukio hilo kwa njia ya Simu afisa elimu
msingi wilayani Geita Mwl.Deus Seif amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na
kuahidi kukutana na kamati ya Shule January 31 mwaka huu ili kutafuta suluhu
kati ya walimu na wananchi.
Walimu waliopigwa
ni Medan
Zacharia na Deograsi Listone ambao wamezungumzia hali iliyowakuta kuwa ni ya
udhalilishaji na kukatisha tamaa na kwamba tangu kuchapwa hawana tena ari ya
kufanya kazi
“Kiukweli
inasikitisha sana na mpaka sasa hatuna tena ari
ya kazi,na kama inawezekana naomba nihamishwe maana inaonakana kama sina
thamani hapa na sijui naponekanaje katika jamii”-alisema mwalimu Medan
Naye Mwl Liston
alisema hata kama itaamuliwa warudi kufundisha
tayari wanafunzi wao watakuwa wakiwadharau ikizingatiwa kuwa walimu hao
hawatakuwa na uwezo wa kudhibiti nidhamu kwa hofu ya kushambuliwa na kupigwa
tena
Kaimu Mkuu wa
shule Mwl.Athuman Augustine anasema Chanzo cha tukio hilo ni walimu kutoa
adhabu ya viboko vitatu kwa kila mwanafunzi ambaye hakwenda kufanya zamu ya
usafi wakati wa likizo na ndipo wakati wa utekelezaji wa adhabu hiyo mmoja wa
wanafunzi waliopewa adhabu akapandisha mapepo hali iliyowafanya wazazi
kughadhabika kuwa huenda hali hiyo imetokana na adhabu
Akizungumzia
tukio hilo ,Katibu wa Chama cha walimu tanzania
CWT wilayani Geita Mwl.John Kafimbi amelaani kitendo kilichofanywa na wananchi
akisema ni fedheha na udhalilishaji katika kada ya Ualimu
www.ngarakwetu.blogspot.com
No comments:
Post a Comment