Watu watatu wanusurika kifo-Ngara
Na.Shaaban
Ndyamukama-ngarakwetublogspot.com
Watu 3 wamenususurika kupoteza maisha baada ya gari walilokuwa wakisaifiria kupata
ajali katika eneo la Murugarama wilayani Ngara mkoa wa kagera wakitoka Nchini
Burundi kwenda jijini Dar es salaam
Tanzania
Ajali hiyo imetolkea Oktoba 23 kwa kulihusisha Gari aina ya
Scania Semi teller lenye no. T949 ADR lenye trela no.T597 ABG mali ya Suleiman
Suri mfanya biashara wa temeke jijini dare s Salaam
Akiongea na ngarakwetublogspot mmoja wa walionusurika katika
ajali hiyo Muuba Mohamed mwenye umri wa miaka 39 amewataja wenzake
waliojeruhiwa kuwa ni pamoja na driver Kassim Mussa 42 na Omary issa 34 wote
wakazi wa Temeke jijini dare s salaam
Mohamed amesema gari hilo lilikuwa likikwepa shimo katikati
ya barabara kutoka kabanga kwenda mjini Ngara, na kwamba gurudumu la nyuma
lilitumbukia katika shimo hilo na kupelekea gari kuyumba ambapo dreva
alishindindwa kumudu usukani wa gari na
Gari kupinduka ukingoni mwa barabara
Amesema majeruhi wote wamelazwa katika Hospitali teule ya
Murgwanza na dreva Kassim Mussa alivunjika mkono na Omary Issa alijeruhiwa
sehemu mbali mbali za Mwili wake
Amesema ajali hiyo ni ya pili kwa gari hilo kufuatia ajali
nyingine iliyotokea Nchini Burundi wakati gari hilo likitoka dare s salaam. Jeshi
la polisi lilithibitisha
Baadhi ya wakazi wa Murugarama wameiomba Serikali kupitia
wakala wa barabara TANROADS kufanya
jitihada za kurekebisha eneo hilo kwani ni eneo korofi na kwamba ajali hiyo ni
ya pili katika eneo hilo na kwamba baadhi ya watu wamepoteza maisha,uharibifu
wa magari na maili
Mmoja wa wakazi wa Murugarama Bw Paul kabona amesema “ikiwa
serikali inajali maisha ya watu kupitia usalama barabarani haina budi kuweka
miundombinu bora, ikiwa ni pamoja na alama za barabarani na kudhibiti mwendo
kasi wa madereva barabarani”
No comments:
Post a Comment