Mwananchi aliyeajiriwa na Mohamed Semdoe, akisafisha Mifuko baada ya kuikusanya |
majaribio ya Godoro |
Mohamed Semdoe,mgunduzi na mtengenezaji wa Godoro |
Mifuko ikiwa katika hatua za awali kutengeneza Godoro |
Godoro likiwa tayari kwaajili ya Matumizi |
MAGODORO YANAYOTOKANA
NA MIFUKO YA PLASTIKI
WAZO LILILOANZISHWA NA
KUBUNIWA NA MKUU WA IDARA YA MAZINGIRA KATIKA WILAYA YA KIBONDO MKOANI KIGOMA
BW.MOHAMED SEMDOE
MHITIMU WA CHUO KIKUU
CHA MZUMBE 2014/15
KIBONDO DISTRICT
COUNCIL
ANAPATIKANA KWA SIMU
NO. 0767830269/0784830269
AU BARUA PEPE mohamedsemdoe@gmail.com
COPYRIGHT@TZ/T/2015/001677 GREEN MATTRESS of MOHAMED SEMDOE
Katika mazungumzo yake na mimi
ameniambia kuwa wazo lake linatokana na kuhakikisha kuwa jamii inapunguza
tatizo la kuzagaa kwa mifuko hiyo,na badala ya kuiacha ikichafua mazingira
ikusanywe na kutengenezea bidhaa inayoinufaisha jamii usika.
Aidha, Bw. Semdoe anasema matazamio yake
ni kuona Miji na vijiji inaepukana na kuzagaa kwa mifuko hiyo ifikapo 2020, na
kama Fedha zikipatikana kwaajili ya kuendeshea mradi huo anategemea kupanua
wigo wa shughuli kutoka katika wilaya ya Kibondo kwa sasa na kufikia maeneo 20
hadi majiji 5,Manispaa 5,Halmashauri 5,na Halmashauri za miji 5 ndani ya
kipindi cha miaka miwili.
Hata hivyo,hadi kufikia sasa amefanikiwa
kutengeneza magodoro 6 ambayo ameyagawa kwa jamii kulingana na mahitaji ya
wahusika.
No comments:
Post a Comment