Baadhi ya viongozi wa Kijiji Kasulo wilayani Ngara watishia
Kujiuzuru
Na:Shaaban
Ndyamukama Ngara
Baadhi ya Viongozi wa
serikali ya kijiji cha Kasulo wilaya ya Ngara mkoani Kagera wametishia
kujiondoa katika serikali yakijiji hicho kwa kupinga kufanya kazi kwa shinikizo
la mamlaka iliyo juu yao bali watatumia sheria kanuni na taratibu katika
kutekeleza majukumu ya wananchi
waliowachagua
Mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Kasulo wilayani
Ngara Yusufu Katula alisema hayo hivi
karibuni wilayani Ngara katika kikao cha serikali yake kilichoitishwa kwa ajili
ya kuweka mipaka kati ya kijiji na mwananchi mmoja kutoka wilayani Geita
aliyeomba ardhi kwa ajili ya makazi na eneo la kufugia mifugo yake kwenye kijiji hicho.
Katula alisema viongozi wa kijiji hicho wamekuwa wakipokea amri kutoka
kwa viongozi wa wilaya ya Ngara na
halmashauri yake kupata ardhi kwa ajili ya kuwagawia watu wao bila kupata Baraka kupitia mkutano
wa wananchi wote. Alisema kwa sasa kijiji hicho hakina ardhi ya kugawa na
aliyepata eneo la makazi Bw Makoye Athumani alituma maombi na kukubaliwa na
wananchi baada ya kuonesha ushirikiano na jamii kwa kuchangia miradi ya kuleta maendeleo
Awali Afisa mtendaji wa kijiji hicho Christopher Nzoya aliwasomea barua wajumbe wa
serikali ya kijiji iliyotoka kwa mkuu wa wilaya ya Ngara kuwa kijiji cha
kasulo kitoe ardhi ekari 50 kwa kampuni
ya Mingo East Africa kwa ajili ya kuwekeza shughuli za kijamii. Barua hiyo
ilifafanua kuwa kampuni hiyo inahitaji ekari
1000 kwa ajili ya kuwekeza shughuli za maendeleo wilayani Ngara na
kwamba serikali ya kijiji cha kasulo
ifanye utaratibu wa kuiwezesha kupata eneo litakalotumika kuanzishwa
miradi mbalimbali itakayowanufaisha wananchi hasa vijana kupata ajira kupitia
kampuni hiyo.
Naye Afisa Mazingira wilayani Ngara Toba Mhina
akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya hiyo alisema viongozi
wa vijiji wazingatie sheria za kugawa ardhi bila kushawishiwa kwa zawadi
ndogondogo kupitia mianya ya rushwa .Mhina alidai kuwa kuna viongozi wasio
waaminifu wanaowazunguka wenzao katika utoaji wa maamuzi hali inayowafanya
wananchi kutuma ujumbe ngazi ya wilaya ili kufuatilia kuwepo rushwa katika
kutoa ardhi kwa waombaji. Mingo East Africa co. LTD iliomba ekari 1000 katika kijiji cha kasulo
wilayani Ngara lakini serikali ya kijiji hicho pamoja na wananchi walidai ekari hizo haziwezi
kupatikana na wala kijijiji hakina mamlaka ya kutoa ardhi zaidi ya ekari 50 kwa
mujibu wa sheria ya ardhi ya mwaka 1999. Kufuatia hali hiyo kampuni ya Mingo ililazimika kupeleka maombi
yake ngazi ya wilaya ambapo ushauri ulitolewa kupewa ekari hamsini badala ya
1000 kwa ajili ya kuanzisha miradi ya kiuchumi jambo ambalo limepingwa vikali
na viongozi pamoja nawakazi wa kasulo
Katika hatua nyingine katika kikao hicho baadhi ya wajumbe
walihitilafiana katika kutoa maoni ya kuweka mipaka ya kijiji na eneo la
aliyeomba makazi na sehemu ya kulishia mifugo yake Bw Makoye Athumani baada ya
kushawishi viongozi kwa kujenga madarasa
mawili kwa shilingi milioni 19 .Samweli
Kapalala Mwenyekiti wa wafugaji na Braiton Mmoja wa wenyeviti wa vitongoji
walisema wanaopewa ardhi wanamaslahi na baadhi ya vigogo wilayani Ngara na
kwamba wanatumia nafasi hiyo kuwanyanyasa wananchi wasio na uwezo kiuchumi hasa
ambao si wafugaji wenye ng’ombe wengi. Maoni ya baadhi ya wajumbe wa serikali
ya kijiji hicho yalimfanya Mwenyekiti wa Serikali hiyo Yusufu Katula kutishia
kujiuzuru wadhifa wake baada ya kumtuhumu kujihusisha na vitendo vya Rushwa
katika utawala wake na kuwanyima
wananchi haki zao za utawala bora. Alisema "Nafanya kazi na
viongozi ambao baadhi yenu mnaendekeza
majungu na kukashifiana nje ya vikao rasmi hali ambayo kwa namna moja au
nyingine inaweza kusababisha uvunjifu wa amani katika kijiji hiki na wananchi
kukosa imani na serikali yao katika kusimamia
maendeleo yao"
Makoye Athumani (Msukuma)kutoka wilayani Geita aliye na
Ng’ombe zaidi ya 700 aliomba ardhi kuwekeza ufugaji katika kijiji cha kasulo na
kujenga vyumba viwili vya madarasa baada ya kuelezwa kuwa kijiji hicho kinao
wanafunzi 400 walioko eneo la Ngoma wanaotembea umbali wa kilomita 27 kila siku
kutafuta elimu katika shule ya msingi Njia panda iliyoko kijijini humo.
Kikao hicho
kilichohudhuriwa na viongozi waandamizi wa halmashauri ya wilaya ya
Ngara ikiwemo Taasisi ya TAKUKURU mbapo mwanasheria wa halmashauri ya wilaya y
angara Kamilius Ruhinda alisema mwenyekiti huyo hana budi kufanya kazi kwa
kuzingatia sheria za utawala bora na unaozingatia demokrasia wa walio wengi
Ruhinda alisema endapo kanuni na taratibu za kugawa ardhi zitafuatwa wananchi
wakahusishwa na nakala za mihtasari za maazimio au makubaliano yakawekewa Baraka
na halmashauri ya wilaya hakutaweza kujitokeza kwa migogoro baina ya viongozi
wa ngazi mbalimbali na wananchi. “Ni jambo la muhimu kila kiongozi ni lazima
kufanya kazi kwa kuzingatia maamuzi ya waliowengi katika utawala bora kuliko
kutumia ubabe katika nafasi yako na
hatimaye kuvunja sheria hili halina budi kufuatiliwa kwa ukaribu na kwa
umakini”. Alisema Ruhinda
Alidai kuwa kufuatia kuhitilafiana katika utoaji wa maamuzi
katika kuhimiza na kuleta maendeleo ya kijiji kuna haja ya Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa
TAKUKURU kufanya uchunguzi dhidi ya viongozi wanaotanguliza maslahi yao kabla
ya wananchi na kukiuka viapo vya kuitumikia jamii.
Hata hivyo mkuu w
wilaya ya Ngara Costantine Kanyasu alipohojiwa na mwandishi wa habari hizi
alisema serikali kazi yake ni kutoa maagizo katika mamlaka zake kutekeleza
baadhi ya matakwa ya wananchi hivyo aliagiza kamati za ardhi kufanya upembuzi
yakinifu kubaini maeneo ya kuweza kuwapatia wawekezaji wazalendo wanaohitaji kufuga kwa njia za
kisasa kwa kuhifadhi na kutunza mazingira. Kanyasu alisema serikali haiwezi
kufanya kazi kwa shinikizo la wachache walio na wivu fitina na majungu na
viongozi wa vijiji wilayani humo wafanye kazi kwa kutii taratibu na kuzingatia mamlaka inayowaelekeza kwa ushauri
kutekeleza baadhi ya majukumu yaliyo na maslahi kwa taifa
No comments:
Post a Comment