![]() |
Wauza mkaa Wilayani Biharamulo |
BIHARAMULO
Serikali mkoani Kagera inatarajia kufanya
msako na kuwaondoa wavamizi wamisitu katika wilaya ya Biharamulo kwa lengo la kuokoa mazingira katika
operation maalumu ijulikanayo kama OMAKA
Zoezi hilo litakuwa chini ya
uangalizi wa Mkuu wa Mkoa kanal mstaafu Fabian Massawe kwakushirikiana na kamati ya ulinzi na
usalama ya mkoa ambo ni pamoja na jeshi lapolisi,magereza,TAKUKURU na Usalama
wa taifa
Akitoa taarifa katika baraza la
Halmashauri ya wilaya ya Biharamulo,kwaniaba ya mkuu wa mkoa Mkuu wa wilaya
hiyo Bw. Lichard Mbeho amesema zoezi hilo
litawahusisha watendaji wa serikali za Vijiji,wataalam wa Idara za ardhi,mifugo
na Misitu
Amesema lengo kubwa ni kuhakikisha
wavamizi wasio kuwa na Vibali wanakamatwa na kuondolewa katika maeneo hayo katika
kata ambazo zina hifadhi ya misitu na wanyamapori
Bw. Mbeho ameyataja maeneo hayo kuwa
ni Rusahunga,Nyakahura,Nyakanazi,Nemba, na kuhakikisha kuwa msako huo
unafanyika kwa usalama bila uwangaji damu
Aidha mkuu huyo wa wilaya ametoa rai
kwa madiwani, na viongozi wengine ngazi za kata kutoa ushirikiano katika zoezi hilo ili kulinda na
kuhifadhi mazingira
Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji
wa Biharamulo Nassib Bakar Mbangga amesema uharibifu ni mkubwa unaotokana na
wananchi kukosa uzalendo hasa ukataji wa miti na upasuaji wambao na ujangiri
katika pori la
Burigi
Imeelezwa kwamba katika mji wa
Biharamulo na maeneo jirani magunia zaidi ya 600 yanauzwa kila siku kwa
kutembezwa na wapanda Baiskeli na Tani mia sita kwa mwezi za mkaa na Mbao
huuzwa wilayani humo na hata nje ya mkoa na wakati mwingine nje ya Nchi hasa
Rwanda na Burundi
Amesema watendaji wake wanafanya kazi
bila uadirifu wakitumia mianya ya rushwa kwa vyeo vyao kuwagawia maeneo
wafugaji kutoka nje ya wilaya hiyo pamoja na wale watokao nje ya Nchi
Aidha Mkurugenzi huyo amesema
hatamuonea aibu mtumishi yeyote wa umaa atakayekiuka taratibu, kwakumchukulia
hatua mbali mbali za kisheria na kwamba watum,ishi hao watoe huduma kwa jamii
kulingana na taaluma zao kwa kutembelea wanachi vijijini na kuepuka kuwa vyanzo
vya majungu
No comments:
Post a Comment