October 31, 2012

Mkoa wangu Kagera ba Dira ya mazingira

Dira ya misitu nchini ni kuimarisha mchango wa sekta ya misitu kwa kuleta maendeleo endelevu ya Tanzania kwa kuhifadhi na kusimamia misitu yake kwa manufaa ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo. Umuhimu wa sekta ya misitu mkoani Kagera umezidi kuongezeka siyo tu katika kuvutia watalii, bali pia katika kutunza mazingira.
Sekta ya Maliasili inajumuisha misitu, ufugaji nyuki, wanyamapori, uvuvi na utalii ni muhimu sana katika uchumi wa mkoa kwa sababu huchangia katika ajira pamoja na kutoa mazao mbalimbali kwa matumizi ya watu hususan nishati. Inakadiriwa kwamba uvuvi na shughuli zinazohusiana na uvuvi huajiri asilimia 6% ya wakazi wa Mkoa wa Kagera.
SEKTA YA MISITU
Mkoa wa Kagera una misitu ya aina mbalimbali kama vile misitu ya asili, misitu ya kupanda inayomilikiwa na wadau mbalimbali kama vile Serikali Taasisi, jamii, wananchi na sekta binafsi. Aidha, misitu ya asili ina eneo la kilometa za mraba 10,148. Misitu iliyohifadhiwa ni 17, na kati ya hiyo 16 ni ya serikali kuu. Ukubwa wa Misitu hiyo ni kilimeta za mraba 3,539.4. Wilaya ya Missenyi ndiyo yenye idadi kubwa ya misitu iliyohifadhiwa, lakini kwa ukubwa wa eneo, Wilaya ya Biharamulo ndiyo yenye eneo kubwa ikiwa ni sawa na 51% ya eneo la misitu ya hifadhi iliyoko mkoani Kagera.
Baadhi ya Misitu hiyo mi kama inavyoonyeshwa kwenye jedwali lifuatalo:-
NA WILAYA JINA LA MSITU ENEO (hekta)
1 BIHARAMULO&CHATO BIHARAMULO
134,000
2 BIHARAMULO NYANTAKARA
26,000
3 BIHARAMULO LUSAHUNGA
9,000
4 MISSENYI MINZIRO
25,000
5 MULEBA RUIGA
4,777
6 MISSENYI MUNENE
5,900
7 MISSENYI RUCHEZI
647
8 MISSENYI BUSHENYI
210
9 BIHARAMULO MABARE
3,000
10 BUKOBA (V) RUASINA
466
11 MISSENYI KIIKURU
600
12 KARAGWE BUGULUGA
1,500
13 KARAGWE BUTALI
1,500
Misitu hiyo ina faida nyingi ikiwa ni pamoja na kuboresha mazingira kuongeza pato la mwananchi, pamoja na kuhifadhi viumbe hai, Aidha kuni na mkaa ni moja ya Vyanzo vya nishati (90%) Nchini. Vilevile misitu inasaidia katika ujenzi wa nyumba na makazi bora ya wananchi. Misitu pia husaidia katika kupunguza gesi-ukaa ambacho na kisababishi kikubwa katika mabadiliko ya tabia – nchi na ongezeko la joto Duniani.
UFUGAJI NYUKI
Ufugaji nyuki hufanyika katika maeneo yenye misitu ya asili aina ya miombo kwa kutumia mizinga ya asili na mizinga ya kisasa. Wafugaji wa nyuki huuza asali na nta ili kujipatia kipato na matumizi mbalimbali kama chakula na dawa.
UTENGENEZAJI WA MIZINGA
MWAKA MIZINGA YA ASILI MIZINGA YA KISASA
 
LENGO
UTEKELEZAJI
LENGO
UTEKELEZAJI
2010/2011
9,000
9,059
300
364
 
UZALISHAJI WA ASALI NA NTA
MWAKA
ASALI
NTA
 
UZITO (Kg)
THAMANI TSHS
UZITO (Kg)
THAMANI TSHS
 
2009/2010
35,645
71,290,000.00
2,990
8,970,000.00
 
MIPANGO YA MATUMIZI BORA YA ARDHI
Serikali za vijiji zimehamasishwa kuandaa mipango shirikishi ya matumizi bora ya ardhi na maliasili.
MWAKA LENGO UTEKELEZAJI %UTEKELEZAJI
2010/2011 Kuhamasisha na kushirikisha vijiji 70 kuandaa mmipango ya matumizi bora ya ardhi na maliasili Vijiji 52 vimehamasishwa na kuandaa mipango ya matumizi bora ya ardhi na maliasili
74%
•  Aidha, Mipaka ya vijiji 590 kati ya vijiji vyote 600 imepimwa.
•  Halmashauri zote zimetunga sheria ndogo za kudhibiti mazingira, na nyingine zimepelekwa Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira ili zihakikiwe na kutiwa saini kwa ajili ya kuanza kutumika.
KUTOA MAFUNZO YA UTENGENEZAJI WA MAJIKO BANIFU
Mafunzo kutengeneza majiko banifu yanayotumia kuni au mkaa kidogo, kwa vikundi mbalimbali vya vijana na akina mama, umetiliwa mkazo ili kupunguza matumizi ya nishati ya kuni na mkaa.
 
MWAKA
LENGO
UTEKELEZAJI
% UTEKELEZAJI
2010/2011 Kutengeneza na kutumia majiko banifu 1,200 Majiko banifu 3319 yametengenezwa na yanatumika
276.6
UVUVI
Eneo kubwa la Ziwa Victoria liko Mkoa wa Kagera (Kiasi cha kilometa za mraba 10,017) ambapo uvuvi wa kati unafanyika. Maeneo mengine ya uvuvi ni katika Ziwa Burigi, Ikimba, Rushwa na Rumanyika. Uvuvi unafanyika pia katika mito ya Kagera, Ngono na Ruvuvu.
Wavuvi wengi wako katika ziwa Victoria hasa wilaya za Muleba ambayo ina 72.8% na Bukoba ina 24.4 ya eneo la ziwa. Eneo dogo la ziwa lipo katika wilaya ya Chato na Bukoba Mjini.
Wastani wa uzalishaji wa samaki katika eneo la ziwa Victoria (Kagera) kutokana na taarifa zilizopo ni karibu tani 27,000 kwa mwaka zenye thamani karibu ya Tsh 2,131,360,000/-. Ili kupambana na uvuvi haramu vikundi 118 vya ulinzi wa mazingira maeneo ya mialo (Beach Management Unit) vimeundwa.
Mkoa una viwanda viwili vya kusindika minofu ya samaki. Kiwanda cha kwanza cha “Kagera Fish Company”cha Kemondo kilianza kazi mwezi oktoba 2003. Kiwanda cha pili “VICFISH Ltd” kilichoanza uzalishaji Juni 2005. Kiasi cha Tshs 614,293,824.33 zimekusanywa kutokana na mauzo ya samaki kgs 4,705,129.68 kwenda nchi mbalimbali za Jumuiya za Ulaya na Afrika.
Aidha, mfanikio mbalimbali yamepatikana katika sekta hii kama vile:-
•  Matumizi ya zana bora za uvuvi yameongezeka kutoka injini 1,077 mwaka 2005 hadi kufikia injini 1,942 mwaka 2010.
•  Katika kuwasaidia wavuvi kutumia maarifa ya kisasa ya uvuvi, wavuvi 286 wamepatiwa elimu ya kufanya uvuvi endelevu.
•  Katika juhudi za kupambana na uvuvi haramu hatua mbalimbali zinachukuliwa ikiwa ni pamoja na :-
Kuendesha doria mbalimbali zilizopelekea wavuvi haramu 324 kukamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria. Kutokana na doria hizo zana haramu zifuatazo zilikamatwa na kuteketezwa: kokoro 317, timba 469, makila 6,089, nyavu za dagaa 146, katuli 6, kwa ujumla zina thamani ya Tshs. 611,395,000/=.
•  Vilevile, zoezi la uelimishaji wananchi limesaidia kusalimishwa kwa hiari zana haramu za uvuvi zifuatazo; kokoro 336, timba 642, makila 1,273, nyavu za dagaa 5, katuli 67, kwa ujumla zina thamani ya Tshs. 316,905,500/=.
UFUGAJI SAMAKI (AQUACULTURE)
Ili kupunguza uvunaji wa samaki katika ziwa Victoria na kuwasaidia wananchi kuongeza kipato na lishe, wananchi wamehamasishwa kuchimba mabwawa ya kufugia samaki. Wilaya ya Ngara mabwawa 220 yamechimbwa, Karagwe 3 na Bukoba 20, Biharamulo 22. Mabwawa haya yanazalisha wastani wa 115MT za samaki kwa mwaka. Changamoto kubwa iliyopo katika ufugaji wa samaki ni uhaba wa vifaranga bora vya kutosheleza mahitaji ya wafugaji wa samaki.
Ufugaji wa samaki umehamasishwa kwa kuwaelimisha wakulima 366 juu ya ufugaji wa samaki katika mabwawa na jumla ya mabwawa 202 yameanzishwa na kupandikizwa vifaranga 37,423 hadi kufikia Juni, 2010.
SEKTA YA WANYAMAPORI
Mapori ni eneo la ardhi lenye mimea na wingi wa anuai ya wanyamapori na/au maji udongo ambao ni muhimu kwa kutunza ukamilifu wa ikolojia iliyopo katika ardhi hiyo.Kuna aina mbili za mapori ambazo ni Mapori ya Akiba na Tengefu na Mapori ya Akiba. Mkoa wa Kagera una aina moja tu ya mapori hayo ambayo ni Mapori ya Akiba. Mapori ya Akiba ni eneo lililohifadhiwa kwa lengo la uzalishaji na uhifadhi wa wanyamapori. Aidha eneo hili huwa lina idadi kubwa ya anuai ya wanyamapori.
Mkoa wa Kagera una mapori ya Akiba matano kama inavyoonyeshwa kwenye jedwali lifuatalo :-
Jina la Pori Mwaka kupanda hadhi Namba ya gazeti la serikali Eneo ( ha)
Biharamulo
1963
GN.No.275 ya 1974
731
Burigi
1972
GN.No.275 ya 1974
2,941
Kimisi
2003
GN No.116 ya 2/5/2003
1030
Ibanda
1974
GN No. ya 1974
294
Rumanyika
1974
GN No.ya 1974
255
JUMLA KUU
5,251
UTALII
Serikali imeboresha barabara katika mkoa kwa kujenga barabara mpya za lami zenye urefu wa km 136. Aidha miundo mbinu ya mawasiliano kama internet na simu za mikononi kwa sasa ipo wilaya zote. Hoteli za kitalii zilizopo ni pamoja na: Walkgard Westland Hotels and Tours, Bukoba Kolping Hotels, Yaasila Top Hotels, Bukoba travelers Inn hotels, Upendo lodge, Spice motels, Coffee tree Inn Hotel na Kamachumu inn.
Wadau wa utalii wameunda na kusajili chama cha utalii kinachoitwa Kagera Tourism Development Association (KATODEA), namba ya usajili ni SO. NO. 12430. Mwaka 2005 KATODEA imeweza kuandaa mpango mkakati wa utalii (Strategic Plan) ambao unaweza kutumiwa kuwavutia wawekezaji katika sekta ya utalii na kuongeza idadi ya watu wanaotembelea mkoa huu kwa shughuli za utalii. Chama hiki kwa kushirikiana na Mkoa kiliweza kuadhimisha siku ya Utalii Duniani kitaifa Oktoba 2006.
Sekta ya utalii inaendelea kukua baada ya kuboresha vivutio vya kitalii mkoani. Idadi ya watalii wa ndani na nje walitembelea mkoa wa Kagera imeongezeka kutoka watalii 602 mwaka 2006/7 hadi kufikia jumla ya watalii 1013 katika kipindi cha mwaka 2009/10, ambayo ni sawa na ongezeko la asilimia 59. Ogezeko hili pia linachangiwa na makampuni yanayojishughulisha na kusafirisha watalii ya Kiroyera Tour Operator na WALKGARD Hotel and Tours.
Vivutio vya Utalii:
Mkoa una vivutio vingi vya kitalii ambavyo huwavutia watalii wa ndani na nje. Vivutio hivyo ni pamoja na maporomoko ya mto Kagera, ufukwe wa kando kando ya ziwa Victoria ambao una mchanga mweupe wa kuvutia, kanisa la Kijerumani lililopo katika wilaya ya Missenyi ambalo lilitumiwa na majeshi wakati wa vita ya Tanzania na Uganda miaka ya 1970, Visiwa mbalimbali ambavyo vinapatikana katika ziwa na aina mbalimbali za wanyama wanaopatikana katika hifadhi ya serikali kama vile nyani.
 CHANGAMOTO ZINAZOIKABILI SEKTA YA MALIASILI
Pamoja na faida kemkem zinazopatikana katika maliasili zilizopo katika Mkoa wa Kagera, changamoto mbalimbali zinatukabili ikiwa ni pamoja na uelewa mdogo wa wananchi katika uhifadhi wa rasilimali hiyo unaosababisha uchomaji moto ovyo wa misitu na nyika, kuongezeka kwa gharama ya nishati ya umeme na gesi kunasababisha matumizi ya kuni na mkaa ,ongezeko kubwa la idadi ya watu na kasi ya kupanuka kwa miji ndani na nje ya mkoa wa Kagera na hivyo kusababisha uvamizi wa Hifadhi za Misituna Mapori ya Akiba kwa shughuli mbalimbali za kibinaadamu zisizoendelevu kama vile :-
•  Uharibifu mkubwa wa mazingira unaosababishwa na uchomaji wa misitu ya asili, ukataji miti ovyo na uchungaji wa mifugo hasa ng'ombe katika misitu.
•  Uharibifu wa mazingira unaofanya na wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu ndani ya msitu wa Hifadhi Biharamulo na maeneo ya Kalugwete na Mavota katika wilaya ya Biharamulo.
•  Tatizo kubwa la uwindaji haramu pamoja na uchungaji wa mifugo unaofanywa na watu kutoka nchi jirani ndani ya Hifadhi za Misitu na Mapori ya Akiba.
•  Upungufu mkubwa wa vyombo vya kufanyia doria katika sehemu za misitu na fedha za kufanyia shughuli hizo.
•  Uwezeshwaji wa vikundi (BMUs) wilayani aidha ni mdogo sana au hakuna kabisa.
•  Kuna upungufu mkubwa wa watumishi wa Sekta zote za maliasili.
•  Kukua kwa soko la samaki katika nchi za Ulaya hivyo imesababisha uvuvi usio endelevu kwa kuvua kupita kiasi, kuvua kwa kutumia zana haramu na uvuvi wa kutumia sumu.
•  Kuimarika kwa teknologia katika viwanda vya kusindika samaki.
•  Kutokuwa na elimu ya kutosha kuhusu uhifadhi wa Maliasili ikiwa ni pamoja na mazingira ya ziwa na uvuvi endelevu miongoni mwa wananchi wa nchi zote tatu waishio kando ya ziwa Victoria.
•  Uvuvi wa zana haramu kama makokoro na nyavu zenye machomadogo (monofilament) zinazotoka nchi jirani pamoja na Kukosekana kwa ‘fishing quotas'
•  Kutokuwa na mipaka inayoonekana ziwani hivyo kusababisha Wavuvi wa nchi moja kuingilia mipaka ya nchi nyingine bila kipingamizi chochote na kufanikisha utoroshaji wa mazao ya uvuvi toka nchi moja kwenda nchi nyingine hasa wakati wa usiku.
•  Wizi wa nyavu, mashine na mitumbwi kuongezeka na wahusika kukimbilia nchi nyingine.
•  Kuwepo na wahamiaji haramu wa nchini wanaojihusisha na biashara ya uvuvi
•  Kutokuwa na usimamizi madhubuti wa pamoja wa sheria za usimamizi wa rasilimali za ziwa miongoni mwa nchi zote tatu. Kwa mfano sheria za kudhibiti uchafuzi wa ziwa ‘lake pollution'
•  Ushirikishwaji mdogo wa wadau wote wanaotumia rasilimali za ziwa katika kusimamia na kuamua masuala yote yanayohusu matumizi na uhifadhi wa rasilimali za ziwa.
JUHUDI ZA KUTATUA MATATIZO
Jitihada mbalimbali zinafanyika ikiwa ni pamoja na : -
•  Mkakati wa kuhifadhi Mazingira ya Ardhi na Vyanzo vya Maji , Halmashauri za Wilaya na Manispaa Mkoani Kagera zinapaswa kutekeleza kwa vitendo Mkakati wa Kuhifadhi Mazingira ya Ardhi na Vyanzo vya maji kama ilivyoelekezwa na Sheria ya usimamizi wa Mazingira ya mwaka 2004 ili kukabiliana na changamoto za uharibifu wa misitu kwa kuibainisha, kuiwekea hatua ya kukabiliana nayo na kuweka mkakati wa utekelezaji utakaozingatia hali halisi ya Wilaya husika
•  Tuzo ya Mh. Rais ya kuhifadhi vyanzo vya maji, kupanda na kutunza miti
Aidha kwa mwaka 2009/10, Mkoa wa Kagera umeshiriki mashindano ya Tuzo ya Mh. Rais ya kuhifadhi vyanzo vya maji, kupanda na kutunza miti na kupata washindi katika ngazi ya Taifa, Wilaya ya Chato na Kata ya Kagongo. Washindi hawa walipokea tuzo hiyo ya fedha taslimu, kombe na cheti kutoka kwa Mh. Rais Jakaya Kikwete siku ya mazingira duniani huko katika mji wa Bahi Dodoma. Kwa sasa tunaendelea na maandalizi ili baadae tushiriki na kuongeza idadi kubwa ya washindi katika ngazi ya Taifa husani katika ngazi ya kaya.
•  Miradi ya usimamizi Shirikishi wa Misitu
Baadhi ya Wilaya za Mkoa wa Kagera kama vile Bukoba, Missenyi na Biharamulo zilipata ufadhili wa World Bank kupitia TASAF na hivyo kunufaika na mpango wa utekelezaji wa Miradi ya Usimamizi Shirikishi wa Misitu (PFM) kwa lengo la kuwashirikisha au kuwamilikisha usimamizi kwa wananchi katika ngazi ya kijiji.
Aidha kwa mwaka wa fedha 2010/11 Wilaya ya Muleba imetengewa kumla ya Tshs. Wa fedha 2010/11 Wilaya ya Muleba imetengewa jumla ya Tsh. 106,000,000/= kupitia ufadhili wa NORAD ili kupunguza uharibifu wa misitu katika eneo hili.
•  Kampeni ya Upandaji Miti Kitaifa, Kimkoa na Kiwilaya
Katika kipindi cha mwaka 2010/11 swala la upandaji miti lilipewa kipaumbele kutokana na kuharibika kwa mazingira ambapo jamii ilishiriki katika kupanda miti maeneo mbalimbali. Takwimu za Utekelezaji wa kampeni ya upandaji miti Kimkoa ulikuwa kama ifuatavyo:-
S/N
WILAYA
LENGO
(Miti)
IDADI YA MITI ILIYOPANDWA
% YA IDADI YA MITI ILIYOPANDWA 2009/10
IDADI YA MITI ILIYOKUZWA
% YA IDADI YA MITI ILIYOKUZWA
1. BIHARAMULO
2,000,000
1,600,000
80%
1.300,400
65%
2. H/BUKOBA
1,500,000
1,114,250
74%
1,100,000
73%
3. KARAGWE
1,500,000
1,265,400
84%
1,250,000
83%
4. BUKOBA (M)
500,000
415,000
83%
402,115
80%
5. CHATO
1,500,000
1,506,847
100%
1,442,760
96%
6. MISSENYI
1,500,000
1,416,500
94%
1,366,310
91%
7. MULEBA
1,500,000
1,859,160
124%
1,805,550
120%
8. NGARA
1,500,000
1,859,160
91%
1,205,550
80%
JUMLA
11,000,000
10,084,607
91%
9,712,535
86%
kwa mwaka 2011/12 kwa kushirikiana na wilaya zote tumelenga kupanda jumla ya miti 11,000,000 katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na vyuo vya elimu na shule, vyanzo vya maji na vilima vilivyokuwa wazi ili viweze kuhifadhiwa.
•  Kupandisha hadhi Misitu ya Hifadhi (National forest Reserve) kuwa Hifadhi asilia.
Mchakato wa kupandisha hadhi misitu wa Hifadhi wa Taifa wa Minziro unaendelea. Kukamilika kwa mchakato huu kutasaidia kuongeza rasilimali za Usimamizi endelevu wa Msitu huo eg; Hifadhi ya Taifa ya Minziro (Nature Reserve).
Aidha juhudi zingine za kuhifadhi maliasili ni pamoja na :-
•  Kuelimisha jamii kutambua athari kubwa zinazotokana na uharibifu wa mazingira.
•  Kufanya doria katika misitu na katika ziwa Victoria.
•  Kufanya operesheni ya kuwaondoa wavamizi wa misitu ya hifadhi na mapori ya akiba.
•  Kutumia sheria zilizopo kuwachukulia hatua wahalifu wanaokamatwa.
•  Kutunga sheria ndogo za usimamizi na hifadhi za misitu, mapori pamoja na rasilimali za ziwa Victoria na vyanzo vya maji katika ngazi zote kuanzia vijijini hadi wilaya.
•  Kuwaelimisha na kuwashirikisha wananchi kikamilifu katika kulinda na kutunza mazingira yao pamoja na kuwafichua wale ambao wanafanya matendo yanayosababisha uharibifu wa mazingira.
•  Ili kuongeza ajira na kipato kwa jamii, wataalamu wa sekta ya Maliasili kwa kushirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali wameendelea kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa kuzalisha mazao ambayo siyo timbao (Non wood products) kama asali na nta.
Kutokana na unyeti wa sekta hii kugusa maisha ya kila siku ya jamii, Vyama Sekta ya Umma na sekta binafsi zishirikiane ili kuweka mikakati ya pamoja ya kukabiliana na changamoto zinazotukabili. Hii itatusaidia kufanikisha shughuli mbalimbali za maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika Mkoa wetu. Kwa kuzingatia Dira ya Taifa ya mwaka 2025, malengo ya Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini (MKUKUTA) 2010, na malengo ya Milenia 2015.

 
Changamoto
Mkoa wa Kagera ni miongoni mwa mikoa nchini inayo kabiliwa na uharibifu wa mazingira. Sababu za uharibifu wa mazingira zinatokana na shughuli za kila siku za mwanadamu kama:
•  Uvunaji wa miti usio endelevu
•  Uchomaji moto misitu
•  Uchungaji wa mifugo katika misitu na mapori ya akiba
•  Kilimo kandokando ya mito na vyanzo vya maji.
•  Kupanda miti isiyofaa kwenye vyanzo vya maji.
•  Uvamizi wa misitu na mapori kwa ajili ya kilimo.
•  Uchimbaji wa madini na kilimo cha kuhamahama
SOURCE:TOVUTI YA MKOA

No comments:

Post a Comment