Maporomoko ya Maji-Rusumo-Ngara |
Na:- Juventus Juvenary-Ngara
Pichani hapo juuni Maporomoko ya maji, yaliyopelekea SERIKALI ya Tanzania, Burundi na Rwanda kutiliana saini mkataba wa maridhiano ya pamoja katika kusimamia mradi mpya na mkubwa wa kuzalisha umeme, kwenye maporomoko ya maji katika Mto Ruvbu uliopo Mkoa wa Kagera hapa nchini.
Mradi huo uliopo chini
ya Uratibu wa Jumuiya ya nchi za Afrika Mashariki (EAC), umefadhiliwa na Benki
ya Dunia (WB), na unatarajia kuzalisha megawati 90 za nishati ya umeme, na
kwamba kila nchi itapata megawati 30 katika mradi huo mkubwa.
Mkataba huo wa pamoja ambao umetiliwa saini jijini Mwanza, umelenga kuchochea zaidi ukuaji wa maendeleo na kupunguza tatizo la upatikanaji wa nishati hiyo, hivyo wanannchi wan chi husika watanufaika na umeme huo
Mkataba huo wa pamoja, umesainiwa na Mawaziri
wa nchi hizo wanaoshughulikia masuala ya Nishati ambao ni Waziri Ngeleja wa
Tanzania, Waziri wa Nchi, Maji na Nishati wa Rwanda, Emmanuel Isumbingabu pamoja
na Waziri wa Burundi anayeshughulikia masuala ya Nishati, Maji na Madini,
Manirakiza Come.
Waziri Ngeleja
aliyataja maeneo hapa nchini yatakayonufaika na mradi huo wa umeme utokanao na
maporomoko ya Mto Rusumo, kuwa ni pamoja na wilaya ya Sengerema na Geita
(Mwanza), Kibondo na Kasulu (Kigoma), pamoja na maeneo ya Mkoa wa Kagera.
No comments:
Post a Comment