Mwanafunzi aliyejifungua wakati wa Mitihani ya Kidato cha nne |
Na Shaaba Ndyamukama Ngara
Mwanafunzi wa kike anayesoma kidato cha nne katika shule ya
sekondari Kibogora wilaya ya Ngara mkoani Kagera amesimamishwa kuendelea na
mtihani wa kuhitimu elimu ya sekondari baada ya kubainika kujifungua siku
chache zilizopita
Mkuu wa shule ya Sekondari kibogora wilayani Ngara Elias
Gozi akiongea na mwandishi wa habari hizi ofisini kwake Jumanne Oktoba 9 alimtaja
mwanafunzi huyo kuwa ni Fausta Emanuel mwenye miaka 17 aliyejifungua siku kumi
kabla ya kuanza mtihani huo ulioanza Oktoba 8 mwaka huu
Gozi alisema mwanafunzi huyo hakugundulika mapema kwa kuwa
alikuwa mtoro wa kuanzia mwezi mei lakini alisajiliwa kufanya mtihani huo wa
taifa na taarifa za kujifungua zilipatikana siku ya mtihani akiwa ameshafanya
somo la Civics shuleni hapo
Alisema kuwa Baada ya wanafunzi wenzake kutoa taarifa za
mwanafunzi huyo kuwa na mtoto mazingira ya nje ya shule uongozi wa shule kwa
kushirikiana na Afisa Elimu Sekondari wilayani Ngara Julius Nestory walimhoji
kuhusu tukio hilo
jambo ambalo alilipinga na kufanya somo la pili la kiingereza
“Nikueleze ndugu mwandishi mimi nina siku chache
nimekabidhiwa shule hii hivyo sikuwa na taarifa yoyote kuhusu mwanafunzi huyo
na inasikitisha hata walimu wazoefu wa
shule hii hawakulieleza hili mapema ili kumkataza kabla ya kusambaa wilayani”Alisema
mkuu wa shule
Elias Gozi aliongeza
kuwa mara baada ya kumaliza somo la pili alitakiwa kutoa maelezo kwa maandishi
ya kukana au kukubali kuwa amejifungua na anaye mtoto mchanga na baada ya
kutafakali kwa kina alikiri kuwa amejifungua siku 10 zilizopita akiwa nyumbani
kwa wazazi wake kijiji cha Bugarama wilayani Ngara
Kwa upande wake Afisa Elimu Sekondari Wilayani Ngara Julius
Nestory alithibitisha kusimamishwa kwa mwanafunzi huyo na kwamba atafanya
mtihani mwakani akiwa ni mwanafunzi wa kujitegemea kwani sheria ya elimu nchini
hairuhusu mwanafunzi wa sekondari kuendelea na shule akiwa na motto kuoa au
kuolewa
Nestory alisema serikali imeanzisha mpango wa elimu ya
masafa kwa walioshindwa kupata elimu ya sekondari kwa kusoma moduli za masomo
kwa muda wa mwakammoja hadi mitatu na wanaweza kufanya mtihani kama wakujitegemea na kupata vyeti vya elimu ya sekondari
Alisema kuwa mwanafunzi wa shule hiyo pamoja na aliyeko
katika shule ya sekondari ya kata ya kibimba wilayani Ngara wanapaswa kupelekwa
katika hospitali na madaktari kuthibitisha
kujifungua kwao na taarifa zao ziambatanishwe kwenye taarifa ya mitihani
No comments:
Post a Comment