Ajinyonga kwa Katani ndani ya Nyumba
Na Shaaban
Ndyamukama Ngara
Mwanamke mwenye miaka 37 mkazi wa kijiji cha Buhororo
wilayani Ngara mkoani Kagera amefariki dunia kwa kujinyonga akitumia kamba ya
katani
Kaimu Mwenyekiti wa kijiji hicho Paulo Bwinyo alimtaja mwanamke
huyo kuwa ni Rejina Semitembe mkazi wa
kitongoji cha Buhororo kati ambaye
alijinyonga jumatano majira ya saa tano mchana akiwa ndani ya nyumba.Bw Bwinyo
alisema kuwa msichana huyo ambaye maishani mwake alikuwa bado kuolewa alipanda
juu ya meza na kutundika kamba katika paa ya nyumba kisha kujitundika baada ya kujifungia ndani ya nyumba hiyo. Alisema wakati wa uhai wake aliishi na mama yake mzazi
mwenye zaidi ya miaka 70 na siku ya tukio mama yake alimuacha nyumbani na kuelekea
shambani na aliporudi alikuta nyumba imefungwa
na alipowaita majirani walikuta mwanae huyo ameshafariki dunia

Naye shuhuda wa pili katika tukio hilo Bi Winifrida Thomas amesema mara baada
ya mama wa marehemu kutoa taarifa kwa majirani kutaka msaada wa kufunguliwa nyumba
yake walifika na kubomoa oukuta karibu na mlamgo wa nyumba na kumkuta msichana
huyo akininginia sebuleni akiwa ameshafariki dunia
Bi winifrida amesema kuwa licha ya kuwa mzima siku za nyuma
lakini tangu mwezi aprili mwaka huu alikuwa akidai kuwa na majini yanayomhubiri
kutafuta kamba ili ajinyonge na alikuwa akiwaeleza watu kuwa iko siku
atajinyonga bila kutoa sababu za kufanya hivyo
Mama yake mzazi na marehemu Bi Marcelina john alidai kuwa
tangu aishi na mwanae alikuwa haoni tatizo lolote la kiafya au kuwa na msongo
wa mawazo ispokuwa moyoni aliwaza kukosa mume kwani hakuna kijana wa kiume
aliyewahi kumuona akiongea na binti yake katika masuala ya mapenzi
Jeshi la polisi wilayaniNgara limethibitisha kutokea kwa
kifo hicho na kwamba linaendelea kufanya upelelezi kuhusiana na tukio hilo.
No comments:
Post a Comment