October 15, 2012

Ngara yaeleza chanzo cha hati chafu

 
 na Ashura Jumapili, Bukoba

CHANZO cha Halmashauri ya Ngara kupata hati chafu kwa miaka miwili mfululizo imeelezwa kuwa imesababishwa na watumishi kufanya kazi kwa mazoea.
Mkuu wa Wilaya ya Ngara, Constantine Kanyasu, alibainisha hayo mwishoni mwa wiki katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa ( RCC) Mkoa wa Kagera wakati Mwenyekiti wa kikao hicho, Kanali mstaafu Fabian Massawe, alipotaka kuelezwa sababu za halmashauri hiyo kupata hati chafu.
Kanyasu alisema wafanyakazi wamekuwa na tabia ya kufanya kazi kwa mazoea kwa kisingizio kuwa watumishi ni wachache, jambo ambalo halina ukweli.
“Binafsi nimeshuhudia baadhi ya watumishi wanaofanya kazi kwa mazoea wala hawamheshimu mkurugenzi ambaye ndiye mwajiri wao,” alisema.
Alisema serikali inapaswa kuwa na utaratibu wa kuhamisha viongozi mara kwa mara, ili kuepukana na tatizo la kufanya kazi kwa mazoea katika halmashauri mbalimbali nchini.
Alisema watumishii katika halmashauri hiyo wana zaidi ya miaka 10 hawajahamishwa, hali ambayo inachangia kuwapo kwa hali hiyo
    na www.freemedia.co.tz/daima

No comments:

Post a Comment