Wajasiriamali wa Ngara wakisubiri Usafiri wa Maloro kupeleka mazao wilayani Kahama mkoani Shinyanga |
Ndizi kutoka Ngara, ambalo ndio zao kuu la Biashara |
Halmashauri Ngara itatue migogoro ya
Ardhi kwa wananchi wake
Na Shaaban
Ndyamukama.Ngara
Halmashauri
ya wilaya ya Ngara mkoani Kagera imeshauriwa kuondoa migogoro ya arhi kwa
wananchi wake kwa kutafuta jingo na kuanzisha baraza la ardhi ili kuondoa
changamoto zinazowakabili wakulima na wafugaji katika halmashauri hiyo
Mbunge wa
jimbo la Ngara Deogratias Ntukamazina
alitoa ushauri huo wakati akiongea na baraza la madiwani hivi karibuni wilayani
Ngarakwa kuelekeza halmashauri hiyo kutafuta mahali palipo karibu na wananchi
kijiografia kujenga jengo kwa ajili ya kuanzisha baraza la ardhi litakalosaidia
wananchi kupunguza kero za mashamba
Bw
Ntukamazina alisema kuwa wananchi
wanayo migogoro ya ardhi wilayani ngara kwa kugombania mipaka ya mashamba na
kusumbuka kutafuta suluhu kwa kulazimika kwenda wilayani chato na hutumia
gharama kubwa kupata haki zao
Alisema kuwa
kama jengo litatolewa na halmashauri wizara ya ardhi na maendeleo ya makazi
itatuma wataalamu wa kulikagua na kutoa ushauri wa maboresho ili kesi mbalimbali
za ardhi ziweze kusikilizwa na kutatua kero zinazowakabili wananchi.“Migogoro
ya ardhi kwa wananchi wetu imekuwa ikisikilizwa na baraza la ardhi la kata
lakini wajumbe wake baadhi yao wamekuwa hawana ujuzi katika sheria na
kusababisha wengi kutaka rushwa na kuwakosesha haki waliozistahili kupata haki
zao kihalali”.Alisema Ntukamazina
Alidai wilaya
ya ngara ina ardhi yenye rutuba na wananchi wanaojishughulisha na kulimo cha
ndizi hasa tarafa za kanazi na Nyamiaga huku tarafa za Rulenge na Murusagamba
wakilima maharage karanga ulezi mtama na matunda mbalimbali pamoja na ufugaji
wenye kulinda na kuhifadhi mazingira.Hata hivyo mbunge huyo aliwasihi wananchi
kutumia vema ushauri utakaotolewa na baraza la ardhi la wilaya litakapopatikana
katika kuhakikisha wanadumisha amani na mshikamano katika vijiji badala ya
kusababisha vurugu kwa watakaoshindwa kupata haki zao kwa mujibu wa sheria.Ends
No comments:
Post a Comment