Mwenyekiti wa CUF taifa- Prof. Ibrahim Haruna Lipumba |
Mwenyekiti
wa Chama cha wananchi CUF Taifa Prof. Ibrahim Haruna Lipumba amekitabilia
vibaya ma Chama cha Mapinduzi CCM kilichoko madarakani hivi sasa kuwa
kitaanguka katika uchaguzi mkuu wa 2015 kwa madai kuwa kimeshindwa kuwaletea
maendeleo Wananchi
Prof.
Lipumba amesema hayo jana wakati akizungumza na Waandishi wa habari wilayani
Kibondo Mkoani Kigoma baada ya kuwaslili wilayani humo akitokea Mjini kigoma
akihitimisha ziara yake Mkoa ya Kigoma
Amesema CCM
kwa sasa kina baadhhi ya Viongozi ambao si waadilifu,wala rushwa na waliopo
madarakani kwa maslahi yao
bnafsi hivyo wanakichafua chama hicho hali inayopelekea wananchi kukosa imani
Ametolea
mfano Vitendo vya Rushwa ambavyo vimekuwa vikiripotiwa kwa nyaakati tofauti
hasa katika chaguzi mbali mbali ikiwa ni pamoja na Uchaguzi ndani ya Chma hicho
uliomalizika hivi Karibuni
Kutokana na
hayo, Prof Lipumba Amesema Vyama vya Upinzani Nchini havina budi kuunganisha
Nguvu kujenga Umoja wa kitaifa, na kujipanga sawasawa ili kuhakikisha
wanakidondosha Chama Cha Mapinduzi katika uchaguzi uja akidai kuwa kimeshindwa kutetea maslahi ya wananchi
Aidha, Prof
Lipumba amesema kuwa CCM kimeshindwa kutimiza ahadi zake kwa wananchi hali
ambayo imepelekea mgawanyiko kati ya wenye mali na Masikini kwa maana ya
kuwepo daraja la wenye nacho na wasiokuwa nacho
Ameongeza
kuwa dawa pekee ya kusuluhisha changamoto zinazowakabili Watanzania ni
kuhakikisha Chama pinzani kinaingia madarakani.
Katika
hatua nyingine mwenyekiti huyo wa Chama cha wananchi CUF Taifa akisema kuwa
anaongozwa na falsafa ya chama chake Vision 4 Change au Ndoto ya mafanikio
amesema Taifa la Tanzania
lina rasilimali nyingi ingawa watanzania walio wengi wanaishi katika maisha ya
Kimasikini
Prof.
Lipunmba amesema njia ya kuwakomboa watanzania wengi ni kupitia Sekta ya kilimo
kwa kuboresha mfumo uliopo hivi sasa
Amesema
Serikali imejaribu kubuni njia za kuboresha kilimo kwa kutamburisha matumizi ya matrekta madogo
maarufu kama power tillers, Pembejeo na Mbolea ya Ruzuku lkn bado kuna changamoto
nyingi kwa kuwa matrekta hayo sehemu kubwa hayafai kutokana na arhi ya sehemu
husika, na Mbolea kuto wafikia walengwa ipasavyo
Kutokana na
maelezo ya Prof lipumba, ili serikali itemize falsafa ya Kilimo Kwanza haina
budi kutumia asilimia 10 ya bnajeti yake ya matumizi yake
Amesema kwa
mujibu wa makubaliano ya Nchi za SADC zilikubaliana kuwa serikali za Nchi
wanachama zinatakiwa kutenga asilimia 10 ya matumizi yote ya serikali katika
sekta ya Kilimo lakini Tanzania
bado haijafanya hivyo
Aidha,mwenyekiti
huyo amesema ili kubooresha sekta ya kilimo Serikali pia haina budi kuweka
vituo vya utafiti wa Kilimo vijijini ili kuwafikia wakulima na kulaani vikali
matumizi mabaya ya fedha zinazotengwa kwaajili ya pembejeo za Kilimo kwani hazitumiki
ipasavyo na badala yake wapo Viongozi wa Serikali wanaotumia fursa hizo
kujinufaisha binafsi. Kwa maslahi yao binafsi. Mwisho
No comments:
Post a Comment