“Ndugu zangu,
Katika pitapita zagu
mitaa ya hapa Bukoba nikalikuta Dukla la Vitabu. Hapo nikakikuta kitabu
kiitwacho " Wanyonge Wasinyongwe". Mwandishi ni Bwana Pius Ngeze.
Nilikisoma kwa siku moja tu. Na katika siku hiyo,jioni, nikakutana na mwandishi
wa kitabu husika, Bw. Pius Ngeze.
Nilifahamu kuwa Pius Ngeze
ni mwandishi wa vitabu na mara nyingine makala za magazetini. Lakini, kuongea
na Pius Ngeze ni sawa na kuingia darasani na kupata maarifa mapya yenye
thamani kubwa. Huyu ni Mtanzania aliyeanza uongozi wa kisiasa akiwa kijana
mdogo wa miaka 34. Ni mwaka 1977 ndipo alipogombea na kushinda nafasi ya
Uenyekiti wa Chama ( CCM) mkoa wa Kagera. Ngeze ni hazina kwa taifa
kutokana na uzefu wake wa uongozi kwa miaka mingi. Kwa sasa amestaafu
uongozi wa kisiasa.
Baada ya kufahamu kuwa
nimenunua na kusoma kitabu chake cha Wanyonge Wasinyonge, basi, Mzee Ngeze
amenipa vitabu vyake vingine viwili; " Silaha 100 Za Kiongozi" na
" Mwanzo Na Mwisho wa Uongozi Wa Kisiasa". Tumepanga tukutane tena ili
tujadili yaliyomo kwenye vitabu hivyo na mengineyo. Inshalah.
Maggid Mjengwa,”
Ndugu mfuasi wa Blog hii. Hayo
ni maneno ya Ndg Maggid Mjengwa aka Kiongozi napenda kumuita hivyo.
Nakushawishi umfuatilie kupitia www.mjengwablog.com
akizungumza kuhusu Mzee Pius Ngeze mzaliwa wa Ngara ambaye Mdau JONAS KIZIMA aliyeko Chuo Kikuu cha
SOKOINE amenitumia taarifa kuwa katika
mahafali ya 28 (yaliyofanyika 23 november 2012 morogoro campus ya mazimbu) ya
chuo kikuu cha sokoine cha kilimo, kilimtunukia ndugu pius ngeze (mzaliwa wa
wilaya ya ngara) nishani ya kutambua mchango wake mkubwa katika sekta ya kilimo
kwa kufanikisha kuchapisha machapisho 57 yanaoelimisha katika sekta ya kilimo
kwa lugha ya kiswahili na kingereza.
No comments:
Post a Comment