Sharlo Millionaire enzi za uhai wake |
Habari zinaeleza kuwa kifo chake
kimetokea Novemba 26(Jana) majira ya saa mbili usiku, ambapo msanii huyo wa
Muziki wa Kizazi kipya maarufu kama Bongo
flavour na mchekeshaji maarufu nchini
Sharo Milionea amefariki dunia kwa ajali mbaya ya gari wakati akitoa Dar es
Salaam kueleka wilayani Muheza, Tanga.
Kwa mujibu wa kamanda wa polisi
mkoa wa Tanga Costantine Massawe Hussein Ramadhani au Sharo Milionea alikuwa
akiendesha gari namba T478 BVR Toyota Harrier. Alipofika maeneo ya Segera gari lake liliacha
njia na kupinduka mara kadhaa, likagonga mti na kusababisha kifo chake na yeye
kutokea mbele ya kioo cha gari na kutupwa mbali.
Alisema Mwili wa marehemu
umehifadhiwa kwenye hospitali Teule ya wilaya ya Muheza. Aliongeza kuwa hakuna
kona kali wala ubovu wa barabara kwenye sehemu aliyopata ajali. Gari lake imehifadhiwa
mahali salama kwakuwa limeharibika vibaya na kwamba kwenye gari alikuwa
mwenyewe.
Mwili wa marehemu baada ya ajali |
Habari kuhusu kifo chake zilianza
kuenea jana usiku ambapo kwa upande wa rafiki yake wa karibu Kitale amesema
alikuwa akiipiga simu ya Sharo Milionea iliyokuwa ikiita kwa muda mrefu bila
kupokelewa na kisha kupigiwa simu na Tundaman, Mzee Majuto na Mjomba wake Sharo
kumtaarifu juu ya kifo hicho.
“Sisi binadamu tunaweza kuwaza hivi
na Mungu naye akawaza lake kwahiyo sisi tunaziombea familia hizi Mungu azipe
faraja ya kweli na faraja ya kweli nadhani inatoka kwa Mungu,” ni kauli ya rais
wa Shirikisho la Filamu Tanzania
, TAFF Simoni Mwakifwamba wakati akizungumza na Shirika la Utangazaji hapa
Nchini TBC.
Umoja wasanii wa filamu nchini
umesema umepata pigo kubwa hasa kwakuwa bado wana msiba wa msanii mwingine wa
filamu, John Stephano ambaye anatarajia kuzikwa leo. Umesema baada ya mazishi
hayo kesho watasafiri kwa mabasi mawili kuelekea wilayani Muheza kwaajili ya
mazishi.
Mungu ailaze mahali pema pepon roho ya Marehemu-Amen
Tunaomba radhi,picha zinatisha
hazistahili kuwekwa wazi
No comments:
Post a Comment