November 23, 2012

RPC KAGERA ATOA TAHADHALI

Kufuatia kitu Kinachosadikika kuwa ni Bomu kuanguka katika Kijiji cha Ruganzo wilayani Ngara mkoa wa kagera,baadhi ya wananchi wameanza kukisogelea,kukigusa na kujariibu kukihamisha huku baadhi ya watoto na wanafunzi wakijaribu kukinyofoa nyuzi.

kufuatia hali hiyo Kamanda wa Polisi Mkoani Kagera Philip Karangi amewataka wananchi kutosogelea eneo hilo wakati huu ambapo Kikosi maalumu kinachohusika na milipuko kutoka dar es Salaam kikisubiriwa.

1 comment:

  1. Inasikitisha kweli. Tangu jana jioni walipoondoka wanajeshi wa JWTZ kwa kile kilichoelezwa kuwa kushindwa kukitambua kitu hicho na kwamba wataalam wengine wa jeshi hilo kutoka D'salaam wako njiani inavyoonekana mamlaka husika hazijachukua serious measures kuhakikisha kuwa kitu hicho kinakuwa chini ya uangalizi wa hali ya juu. Ni aibu hata kwa viongozi wa serikali ya mtaa/Kitongoji au ya Kijiji hicho pia kushindwa hata kusimamia tahadhari hiyo. Yaani hata wazazi ambao ni watu wazima wameshindwa kuwazuia watoto wao wasikichezee kitu hicho!?

    ReplyDelete