HALMASHAURI
YA WILAYA BIHARAMULO KUTUMIA SHILINGI
BILIONI
19,314,305,400
KWA MWAKA WA FEDHA 2013/14.
Halmashauri ya wilaya ya Biharamulo Mkoani kagera imekisia
kutumia zaidi ya shilingi bilioni 19.3 katika
utekelezaji wa miradi ya maendeleo
ambazo zitatokana na wahisani mbali mbali,ruzuku ya serikali na vyanzo
ya ndani
ya halmashauri hiyo kwa kipindi
cha mwaka wa fedha wa 2013 na 2014
Akisoma mapendekezo
ya bajeti kwa mwaka 2013/14mweka
hazina wa halmashauri hiyo Bw. Alexandar Bashaura amesema kuwa katika bajeti hiyo kiasi cha shilingi bilioni 4 zinatarajia kutumika katika utekelezaji wa
miradi ya maendeleo.
Bw. Bashaura amesema kuwa kiasi cha
shilingi bilioni 10.9 ambazo ni sawa na asilimia 57 zitatumika katika kulipia
mishaharara na bilioni 3 .4 zitatumika
kwa matumizi mengineyo
Hata
hivyo makisio hayo ya bajeti kwa mwaka wa fedha 2013/14 ina ongezeko la
shilingi bilioni 3, milioni 143, na laki
7 na 37 elfu sawa asilimia 20 ikilinganishwa na bajeti ya 2012/13 ambapo
makisio yalikuwa shilingi Bilioni 16,milioni 170, laki 5 na sitini na 7 elfu.
No comments:
Post a Comment