Picha kwa hisani ya Mdau Prosper Kwigize akiwa lake Tanganyika Kigoma-STANDARD RADIO FM-TANZANIA |
WAKATI
MAADHIMISHO HAYO YAKIFANYIKA WILAYANI BIHARAMULO:-
Chama cha Mapinduzi CCM kimewataka wanachama na wafuasi wake
kutumia siku ya maadhimisho ya miaka 36 tangu kuanzishwa kwa chama hicho
kufanya tathimini ya mafanikio na kuweka mikakati ya kukiboresha kwaajili ya
maendeleo ya wananchi
Wito huo umetolewa na Katibu wa CCM wilayani humo Bi. Odilia
Francis Maholero wakati akizungumza na radio Kwizera Mjini Biharamulo
Bi. Maholero amesema maandalizi ya sherehe za maadhimisho ya
siku ya kuzaliwa kwa CCM yanaendelea vizuri ambapo wilayani humo,sherehe hizo
kiwilaya zitafanyika katika kata ya Kabindi
Hata hivyo maadhimisho hayo wilayani humo,yamefanyika
Februari 4 wakati kilele kikiadhimishwa Februari 5, ikiwa ni miaka 36 tangu Chama
hicho kilipozaliwa Februari 5 mwaka 1977
Kwa upande wake mwenyekiti wa chama hicho wilaya ya
Biharamulo Bw. Dominick Kasigwa amesema wanachama wa CCM wakienzi chama chao
kwa kufanya kazi hasa kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo katika jamii,
hali itakayoepusha malalamiko kwa jamii kuwa serikali imewatelekeza
Katika hatua nyingine,ametoa wito kwa wananchi kuwa na mwamko
wa kuhudhuria vikao na mikutano mbali mbali ya hadhara ambayo ndiko chimbuko la
maendeleo,hasa pale jamii inapotakiwa kubuni na kuibua miradi ya maendeleo
Mgeni rasmi katika shughuli hiyo alikuwa Mkuu wa wilaya hiyo Bw. Lichard Mbeho ambaye katika hotuba
yake amewaka wananchi kuacha malumbano ya kisiasa hasa itikadi za vyama vingi
badala yake waelekeze nguvu katika kufanya kazi.
Je,huko uliko
wewe,maadhimisho hayo yalikuwaje? Tuma picha,habari na matukio hapa. www.juveilla@gmail.com
No comments:
Post a Comment