|
Baadhi ya maafisa watendaji wilayani Muleba wakizijaribu pikipiki walizogawiwa |
|
Baiskeli kwajili ya wahudumu wa afya Vijijini |
|
Mwenye tai nyekundu ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Muleba Bw.George Katomelo |
Mwenyekiti wa halmashauri Bw.George katomelo akikabidhi Pikipiki
|
M/Kiti wa halmashauri akizungumza na Vyombo vya habari baada ya mgao huo |
|
Diwani wa kata ya Muleba Mjini Bw. Hassani Millanga |
|
Wahudumu wa afya vijijini wakipokea Baiskeli za Kazi |
|
Maafisa watendaji wa kata wakiwa tayari kuondoka na Pikipiki zao |
|
Kushoto ni Afisa habari wa Halmshauri ya Muleba |
|
madiwani wa H/W Muleba katika moja ya Vikao vya Baraza lao |
|
Mwenye shati jeupe ni Charles Mwijage Mb. wa Muleba kaskazini akiwa katika kikao cha Baraza |
|
Majengo ya Ofisi za halmashauri ya Muleba yakikarabatiwa |
|
Wakuu wa Idara ya H/W Muleba wakisoma makablasha ya Kikao |
Watumishi wa kata na vijiji wapatiwa vyombo vya usafiri
Muleba
Na Shaaban Ndyamukama Agost 05,2013
MULEBA: HALMASHAURI ya Wilaya ya Muleba mkoani Kagera imewapatia vyombo vya usafiri watumishi
wake ngazi ya kata na vijiji ili waweze kutekeleza majukumu na malengo ya
halmashauri hiyo kuleta maendeleo ya
wananchi kwa haraka.
Mkurugenzi wa Halmashauri wa wilaya hiyo Oliva Vavunge
amesema hayo Agosti 01,kuwa watendaji wa
kata 18 wamepatiwa pikipiki zenye thamani ya Tsh. 39 mil na wahudumu wa Afya
vijijini 45 wamepatiwa Baiskeli
zilizogharimu Tsh.8.1 mil
Vavunge amesema kuwa
fedha zilizotumika kununua vyombo hivyo vya usafiri ni kutoka katika mapato ya
ndani ya halmashauri hiyo na watumishi
hao wamekopeshwa na watakuwa wakikatwa fedha kutoka katika mishahara yao
ili kwa awamu nyingine watendaji wa kata 13 waweze kukopeshwa
Aidha amesema halmashauri kupitia idara ya kilimo imenunua
trekta kwa kiasi Tsh.milioni 42 ambapo kwa atakayelihitaji kulitumia kwa kilimo
na atalikodi kwa ekari moja Tsh.60,000/=.
Naye Afisa mtendaji wa kata ya Biirabo Boaz Musasa
ameshukuru kwa niaba ya wenzake kupatiwa pikipiki na kwamba katika kata yake
amehudumia vijiji vyenye maeneo mapana yaliyo na mabonde na milima.
Akikabidhi vyombo
hivyo Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Muleba Bw George katomelo
amewahimiza kuhakikisha watumishi hao wanavitumia kwa malengo yaliyokusudiwa
licha ya kuwa mali yao baada ya makato katika mishahara yao. MWISHO
No comments:
Post a Comment