Na Shaaban Ndyamukama Agost 06,20013
MULEBA:WANANCHI wa kata za Rutoro
na Ngenge katika wilaya ya Muleba Mkoani Kagera maisha yao yako hatarini baada
ya kuvamiwa na wahamiaji haramu na wenye mifugo kisha kulishiwa mashamba yao
Mbunge wa jimbo la MULEBA Kaskazini
Charles Mwijage ameliambia gazeti hili jana kuwa wahamiaji hao waliingia katika
kata hizo tangu Rais Kikwete atoe agizo la wahamiaji haramu kuondoka
nchini ndani ya siku 14 kabla ya kuanza
msako dhidi yao
Mwijage amesema kuwa mifugo
iliyoshambulia mashamba ya wananchi wa kata hizo ni takribani 300 na walitokea eneo la pori la burigi kilomita
45 kutoka karika kata hizo
Alisema kuwa wananchi kwa sasa
watakumbwa na janga la njaa kwani mazao waliyokuwa wakitegemea katika yameliwa
na mifugo hiyo na wengine wanadhaniwa kuwa majangiri wanaoingia katika hifadhi
na kupora maliasili za Taifa
“Ifanye nguvu za ziada katika
kuwaondoa wahamiaji haramu kwani wana mtandao mkubwa na wanaendelea kuwa na
dharau hata kwa na vyombo vyake vya
dola”
Amesema pia wahamiaji hao
wanatishia maisha wanaowanyoshea vidole na kuwakemea kupitia mikutano ya
wananchi hivyo ni jukumu la serikali kuhakikisha watu wa namna hiyo wanatiwa
kwenye mkondo wa sheria
Kwa mujibu wa Mbunge huyo ni kwamba
amemtaarifu waziri mkuu na wizara ya mambo ya ndani kuhaikisha wanaimarisha
usalama wa raia na mali zao pasipo kutafuta maneno kupitia majukwaani
Hivi karibuni Rais Kikwete akiwa
ziarani mkoani Kagera alitoa siku 14 kwa wanaomiliki silaha kinyume cha sheria
kujisalimisha na silaha zao ama kuondoka nchini hasa katika mikoa ya Kagera na
Kigoma
Inakadiliwa mkoani Kagera unao wahamiaji haramu zaidi ya 35 000 na
wamekuwa wakishirikiana na watanzania wasio waaminifu kimaadili na kuteka
magari kisha kupora mali za abiria pamoja na
wenye mifugo kuharibu mashamba ya wakulima. MWISHO
No comments:
Post a Comment