August 23, 2013

MKUTANO WA CHADEMA-NGARA August 17,2013 UWANJA WA POSTA YA ZAMANI MJINI NGARA

Mbunge wa Biharamulo Magharibi Dr.Anthony G.Mbassa akiwapanga watu kupisha Helkopita kutua

Helkopita ya CHADEMA ikiwa angani

inakaribia kutua

Inakaribia kutua Uwanja wa Posta ya zamani

imesogelea uwanja

Ikiwa uwanjani,muda mfupi kabla ya viongozi kuteremka

M/kti wa CDM Taifa Freeman Mbowe akiongozwa na M/kiti wilaya Essau Hossea Chiza

Freeman Mbowe akihutubia wananchi

Mnadhimu mkuu wa kabi ya upinzani Bungeni na mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu akihutumia wananchi

John John Mnyika,mbunge wa ubungo na Mkurugenzi wa habari na mawasiliano wa Chadema akihutubia wananchi-Ngara

Makamu mwenyekiti wa CHADEMA kanda ya ziwa magharibi na Daktari Bingwa wa Buganso Dr.Kabangila Rodrick

Dr.Gresmus Ssebuyoya. Mganga Mkuu wa Hospitali teule Biharamulo akiwa katika Mkutano wa CHADEMA wilayani Ngara kutoa elimu kwa wananchi juu ya rasimu ya  Katiba mpya

Baadhi ya mali za wanachama wa CCM waliokihama chama hicho na kujiunga na CHADEMA

M/kiti wa CDM Taifa Freeman Mbowe akipokea kadi za wana CCM na mali zao kabla ya kuwakabidhi Kadi na baadhi ya Nyaraka za CHADEMA

Baadhi ya wana CCM baada ya kuvaa rasmi nguo na kukabidhiwa kadi za uanachama wa CHADEMA


Baadhi ya wafuasi na waliowahi kushika nyadhifa za uongozi katika vyama vya siasa kikiwemo chama cha Mapinduzi CCM wamekabidhi kadi zao na kujiunga na chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA

Wafuasi hao wa vyama vya Siasa wamejiunga na CHADEMA na kukabidhi kadi zao kwa mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Bw. Freeman Mbowe katika mkutano wa hadhara uliofanyika Mjini Ngara mwishoni mwa wiki iliyopita

Miongoni mwa wafuasi hao ni pamoja na Bw. Kennedy Stanford aliyekuwa mwenyekiti wa NCCR Mageuzi,Bi. Elda Ruhimbizi aliyekuwa mjumbe wa mkutano mkuu wa taifa jumuiya ya wanawake CCM, na Magdalena Ntazimila aliyehama kutoka chama cha Mapinduzi

Mwingine ni Mwenyekiti wa kata ya Rulenge kupitia chama cha mapinduzi CCM Bw. Philimon Charles.

No comments:

Post a Comment