-MWENYEKITI CHADEMA KAGERA:-HAKUNA KIZUIZI KWA CHADEMA
KUINGIA IKULU
Chama cha Demokrasia na Maendeleo
CHADEMA wilayani Ngara kimemchagua aliyekuwa mwenyekiti wa NCCR Mageuzi
Bw.Kennedy Stanford kuwa mwenyekiti wa
chama hicho
Bw.Stanford ameukwaa uenyekiti
huo,kufuatia Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema wilaya ya Ngara Mkoani
Kagera kufanya uchaguzi na kupata viongozi wa kikatiba watakaokiongoza chama
hicho kabla ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwakani
Katika uchaguzi huo uliofanyika
Oktoba 19,2013 katika ukumbi wa Paradise mjini Ngara na kusimamiwa na
Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Kagera Bw. Wilfred Lwakatare, mwanachama mpya wa
chadema Bw Kenedy Stanford ambaye alihamia rasmi CHADEMA mwezi August mwaka huu na kukabidiwa kadi ya
uanachana na mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Mh. Freeman Mbowe amechaguliwa kuwa mwenyekiti baada ya
kujiuzulu kwa Bw Essau Hosea Chiza
Nafasi ya Katibu imechukuliwa na Bw
Filmon Charles huku Bw Nestory Mashishanga akibaki katika nasafi yake ya
mwenyekiti wa Baraza la Vijana la chama hicho na Katibu mwenezi akibaki Bw
Wilson Kakoko
Aidha uchaguzi huo umehudhuriwa na
wajumbe 103 kutoka kata 17 kati ya 20 za wilaya ya Ngara ambao wameshiriki
kupiga kura kwa viongozi hao
Akizungumza baada ya Uchaguzi
huo,mwenyekiti wa Chadema Mkoani Kagera Bw. Wilfred Mugisha Lwakatare amesema
kupatikana kwa viongozi waliochaguliwa kutaimarisha nguvu ya chama hicho na
kuhakikisha ushindi katika uchaguzi mkuu ujaop kuanzia ngazi za vijiji
,kata,jimbo na uraisi
“Hakuna kizuizi tena kwa CHADEMA
kwenda Ikulu,miongoni mwa maeneo ambayo CHADEMA Haikuwa na nguvu sana ni Ngara.
Ila kwasasa Chama hiki kimeshika kasi,na kufikia uchaguzi mkuu tutakuwa na
nguvu zaidi,kwahiyo ushindi ni wa CHadema kwa ngazi zote” alisema
Aidha,Bw. Lwakatare amewapongeza
wanachama wa chama hicho kwa namna wanavyojitoa kuimarisha chama chao,akiongeza
kuwa hata katika uchaguzi huo wajumbe wamejisafirisha kwenda na kurudi,bila
kudai posho
No comments:
Post a Comment