October 24, 2013

MWENYEKITI CHADEMA NGARA ASEMA USHINDI NI WA CHADEMA 2014/15



Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Ngara Bw.Kennedy Stanford

Akizungumza na www.ngarakwetu.blogspot.com

akiwa katika moja ya studio za Radio Kwizera mjini Ngara

Akifanya mazungumzo na Radio Kwizera
 Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema wilayani Ngara Bw. Kennedy Stanford amesema CHADEMA wilayani Ngara imejipanga vizuri kuhaikikisha wanalinyakua jimbo hilo kutoka mikononi mwa CCM

Mwenyekiti huyo ameiambia Ngarakwetu kuwa, kwasasa Chama hicho kinaendelea kuimarika zaidi kwakufanya uchaguzi katika kjata ambazo hazimaliza uchaguzi wa viongozi wa chama hicho

Amesema, hiyo yote ni mikakati kuhakikisha kuwa ushindi kuanzia ngazi za vitongoji, Vijiji,udiwani ,ubunge na Urais unakwenda kwa CHADEMA

Aidha, mwenyekiti huyo wa Chadema ametoa wito kwa wananchi kujiunga na CHADEMA kwakusema kuwa ndio chama pekee chenye uwezo wa kutatua changamoto zinazowakabili wananchi wilayani humo.

No comments:

Post a Comment