Dk Peter Bujari. Picha kutoka Maktaba |
DK Bujari wakati wa kampeni kuelekea uchaguzi mkuu 2010. Picha kutoka Maktaba |
Na, Juventus Juvenary
ALIYEKUWA mgombea ubunge jimbo la Ngara
kupitia Chama cha Mapinduzi CCM katika uchaguzi mkuu uliopita 2010 Dk. Peter
Bujari ametangaza rasmi kukihama chama chake na kujiunga na chama cha
Demokrasia na maendeleo CHADEMA
Akizungumza na wandishi wa habari
nyumbani kwake katika kijiji cha Bikiriro wilayani Ngara,Dk Bujari alisema ameamua
kujiunga na CHADEMA baada ya kuridhishwa na sera na uwajibikaji ndani ya chama
hicho
Alisema kuwa atakabidhi kadi ya CCM kwa
Mwenyekiti wa CHADEMA taifa Bw. Freeman Mbowe ambaye anatarajiwa kuwa wilayani
Ngara Jumamosi Disemba 28 mwaka huu
Awali taarifa kutoka kwa mwenyekiti wa
Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA Bw. Stanford Kennedy Festo zililidokeza
gazeti hili kuwa Dk. Bujari alikuwa na mpango wa kuhamia Chadema na kwamba
suala hilo lingetangazwa rasmi baadae
Hata hivyo alisema kuondoka kwake CCM
na kwenda CHADEMA ni kutaka kuleta mabadiliko katika upinzani dhidi ya Chama
cha Mapinduzi, na kwamba atahakikisha kuwa wafuasi aliokuwa nao wanahamia
kwenye chama hicho
Dk Bujari alisema Chama cha Mapinduzi
CCM kina muda mrefu tangu kuanzishwa kwake lakini kimeshindwa kuwajibika na
kuwaletea maendeleo wananchi hali ambayo yeye kama mzalendo hawezi kuivumilia.
No comments:
Post a Comment