Siku chache zilizopita baada ya Ulimwengu kupata taarifa za
kifo cha aliyekuwa Rais wa Afrika ya Kusini Nelson Mandela,baadhi ya watu
wakiwemo wanasiasa hapa Nchini wameonesha kuguswa na kifo hicho
Miongoni mwao wametaja kifo hicho kuwa ni pengo lisilozinbika
kirahisi katika harakati za ukombozi, na jitihada za kuharakisha maendeleo.
Miongoni wa walioonesha kuguswa na kifo hicho ni Dk. Anthony Gervase Mbassa
Mbunge wa jimbo la Biharamulo magharbi (CHADEMA) anayewataka watanzania kila
mmoja kwa nafasi yake kutimiza wajibu
wake katika majukumu aliyonayo na kumuenzi MANDELA kwa kuyatenda mema yote aliyokuwa akiyapigania.
Haya ndiyo aliyosema:-
Hakika kifo ni safari tarajiwa ya kila mmoja na hakuna
awezaye kuiepuka japo kwa gharama yoyote ikiwa Mwenyezi Mungu amependa kukuita
kwake.
Leo tena tunashuhudia ukomo wa miaka 95 wa nyota iliyoleta
nuru, upendo, mshikamano wa dhati katika kuupinga ubaguzi wa rangi ikipoteza
nuru yake barani Afrika ! Hakika nuru imezimika.
Dk. Mbassa anasema Imemchukua muda kuamini taarifa hizi, japo kama si tarehe mosi April kila mwaka siku ambayo watu huitumia kudanganyana kwa muda, lakini mara nyingi taarifa ya kifo huwa haina utani wa jinsi hiyo.
“Nikakumbuka kwa kina safari ndefu mpambanaji huyu, mtetezi
wa haki za binadamu jinsi alivyopitia hatua ngumu zenye kumuhitaji mtu kufanya
maamuzi ya kina na ya dhati katika kupambana na harakati za ukombozi wa walio
wengi.” ansema ni ngumu kuamini kutokana na umuhimu wake licha ya kuwa taarifa
za kuugua kwa mzee Mandela zinafahamika
Mara nyingi watu hawa maarufu jitihada zao huonekana mapema
sana katika maisha yao ya kila siku na mwisho huwa wanashuhudia kwa kiasi
kidogo mafanikio ya juhudi walizo zifanya. Na hakika huo ndio ukweli wa
mashujaa wengi wanaojitoa katika kuleta ukombozi.
Historia ya Madiba inaazia mbali, kama kijana pekee ambaye kwenye familia yake ndiye aliyepata bahati ya kupata elimu enzi hizo za utawala wa ki -chief ili akafanye kazi kwa chief, lakini anaponyoka mkondo huo na kujikuta akiingia chuo cha elimu ya juu katika chuo kikuu cha Fort Hire kwa watu weusi kipindi hicho, pamoja na kuchaguliwa kuwa kiongozi wa serikali ya wanafunzi alijikuta akisimamishwa chuo baada ya kuunga mkono madai ya walio wengi kutaka kuboreshewa hali ya chakula na mazingira ya chuo.
Hakika hii ni kujitoa kwa moyo wa dhati.
Kana kwamba haitoshi, baada ya kuhitimu kama mwanasheria,
anaitumia elimu yake pamoja na wachache waliokuwa wamepata elimu kipindi hicho
kwa manufaa ya jamii nzima, lakini kwa maksudi serikali ya kidharimu ikaamua
kufunga ofisi hiyo na kuihamishia mbali watu wasikoweza kufika kwa urahisi, hii
ni kuendeleza ukandamizaji wa haki za Binadamu.
Pamoja na misukosuko mingi ya kufungwa jela kisa kasafiri
bila kibali, masuala yote ya kuwekewa kesi kama uhaini na mwisho kufungwa jera
miaka ishirini na saba ni sadaka ndefu sana kwa maisha ya mwanadamu.
Na hakika baada ya yote hatukuwahi kusikia kesi yoyote akidai
fidia kwa mateso aliyopata akipinga ubaguzi wa rangi.
Ni somo kubwa sana kwetu sisi tuliobakia, nina uhakika kama lingemtokea sasa hivi mtu ambaye hakuzaliwa na chembechembe za uzalendo hakika kulipiza kisasi ingekuwa ndiyo suluhisho la mambo yote.
Kubwa ni kila mmoja atimize wajibu wake katika majukumu
aliyonayo mbele ya safari, na tumuenzi kwa kuyatenda yote aliyotuachia. Nina
imani katika nyanja zote kauugusa iwe ki-imani, ki-siasa, ki-uchumi,
ki-saikolojia nk. Je mimi na wewe mchango wetu katika nchi yetu ni upi?
Tafakari!
No comments:
Post a Comment