Dk. Ssebuyoya akiwa na wajumbe wa kamati ya CHADEMA wilaya, wakifuatilia mkutano |
Mwenyekiti wa tawi la Mukabenga akifungua mkutano |
Kutoka kushoto ni Bi.Elda Brighton,Katikati ni Dk. Gresmus Ssebuyoya na kulia ni Bi.Magdalena Ntazimila katika mkutano wa hadhara -Mwivuza |
NGARA
Wajumbe wa kamati kuu ya chama cha
demokrasia na maendeleo Chadema wilayani Ngara wamewataka wananchi wilayani
humo wenye sifa za kuchagua na kuchaguliwa kuwa viongozi kutumia kujitokeza kwa
wingi katika uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu ujao
Wajumbe hao Dr. Gresmus Ssebuyoya
na John simon Malanilo wametoa wito huo kwa nyakati tofauti katika mikutano ya
hadhara iliyofanyika katika Vijiji vya Mwivuza na kirushya
Akizungumza katika mkutano
uliofanyika katika kitongoji cha Mukabenga,mmoja wa wajumbe hao Bw. John Simon
Malanilo amesema ni haki kwa kila mwananchi kuchagua na kuchaguliwa
Kwa upande wake Dk. Gresmus
Ssebuyoya amesema kupitia chaguzi hizo,CHADEMA itapata viongozi makini
watakaoharakisha maendeleo ya jimbo la Ngara,hivyo ni fursa kwa wananchi
kushiriki kikamilifu.
No comments:
Post a Comment