Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikan Tanzania Dk.Jacob Chimeledya ametaka
serikali kufanya marekebisho baadhi ya sheria ambazo zimekuwa kandamizi
kwa jamii pamoja na kuiangazia upya mikataba yote inayohusu rasimimali za umma
yakiwemo madini ili ziwe na manufaa kwa wananchi.
Askofu Chimeledya ametoa kauli hiyo kwenye ibada ya
kuzindua dayosisi Mpya ya Biharamulo na kuwekwa Wakfu kwa Askofu wa kwanza wa
Dayosisi hiyo Askofu Vithalis Yusuph.
Bila kutaja sheria husika ,Alisema baadhi ya sheria zikiwemo
sheria paamoja na mikataba iliyoingiwa na serikali inaumiza wananchi na hivyo
ifaa ifanyiwe marekebisho ili rasilimali hizo ziwanufaishe wananchi.
Alisema Tanzania bado ina mikataba mibovu hasa katika sekta ya
madini kwani rasilimali hizo haziwanufaishi wananchi kama zilivyotolewa na
mwenyezi Mungu kwa ajili wanadamu.
Alishauri serikali kuwa, kama kuna mikataba iliyoingiwa ni
mibovu heri ikafanyiwa marebisho kuliko kuendelea kupoteza rasilimali nyingi za
watanzania kwa manufaa ya watu wachache.
Aidha kusuhu sheia za mwanamke Askofu huyo alisema katika sheria
nyingine mbovu ni sheria ya motto hasa wa kike ambapo baadi yake zimekuwa
kandamizi kwa motto wa kike kwani zimekuwa hazimlindi mtoto wa kike katika
mazingira ya leo na hivyo kuwa kandamizi kwake.
“Tunaomba sheria zirekebishwe zikiwemo za kulinda haki za mtoto
wa kike katika mazingira ya leo.Tunaona baadhi ya sheria haziendani kabisa na
utu wa kibinadamu na zimekandamizi kwa mtoto hasa wa kike”alisema Askofu.
Hata hivyo,alisema kanisa linaunga mkono juhudi za serikali
inayoongozwa na Rais John Pombe Magufu katika kupigania rasilimali za nchi
yakiwemo madini,na kuongeza kuwa kanisa litaendelea kumuombea.
“Tunatambua kazi nzuri zinazofanywa na rais Wetu Magufuli za
kupigania rasimali za nchi,lakini cha msingi tunaomba kasoro zilizopo kwenye
mikataba ya madini na sheria zingine mbovu zifanyiwe marekebisho…zipo kanuni
nyingi ambazo zimetumifika hapa tulip oleo”alisema Askofu.
Aidha,Askofu wa Dayosisi ya Biharamulo katika Hotuba yake mara
baada ya kusimikwa kuwa Askofu wa Dayosisi hiyo ya 28,alisema Watanzania walio
wengi wanaishi katika mazingira magumu na ili kuondokana na hali hiyo Viongozi
wa dini na serikali wana wajibu wa kuwahudumia wananchi kwa ushirikiano.
Katika kuonyesha kukerwa na tabia za utumikishwaji wa
watoto,Askofu Yusuph alisema, kanisa la Angilikani Dayosisi ya Biharamulo
halitakubali kuona motto anatumikishwa katika ajira hatarini za migodini,kwenye
migahawa na kuchunga mifugo.
Akizungumzia changamoto za wananchi wa Biharamulo mbele ya Mgeni
Rasim Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga,alisema
wakazi wa wilaya hiyo wanakabiliwa na tatizo la upatikanaji wa huduma ya maji
safi na salama.
Alisema kutokana na hali hiyo baadhi yao wamekuwa wakishinda
usiku wamanane wakitafuta huduma ya maji sehemu mbalimbali na hata maji
wanayotumia hayako salama kwa ajili ya Afya zao.
Aliongeza kuwa kanisa litashirikiana na serikali kuhakikisha
huduma ya maji safi na salama kutoka Ziwa Victoria inapatikana kwani kanisa
hilo linatambua juhudi za serikali za kuwaletea wananchi maendeleo.
Kwa upande wake Mgeni Rasmi Ezekiel Kyunga ambaye pia ni Mkuu wa
mkoa wa Geita aliyemwakilisha Rais wa John Pombe Magufuli katika Hafla hiyo
alisema,serikali itahakikisha inashughulikia kero za wananchi na kuwataka
viongozi wa dini kutoa ushirikiano katika mkakati wa serikali ya awamu ya tano
ya kuwaletea wananchi maendeleo.
Amewataka vongozi dini kuhakikisha wanatumia nafasi zao katika
kueneza injili ili kuwa Taifa lenye kumpendeza Mungu na kupunguza uharifu
unaojitokeza.
Kuhusu maji,alisema serikali iko tayari kushirikiana na kanisa
hilo kuhakikisha wananchi wa Biharamulo wanapa huduma ya maji safi na salama,na
kudai kuwa anatambua juhudi za kanisa hilo kutumia rasilimali fedha kuwahudumia
wananchi ikiwemo elimu,Afya na Maji.
Shughuli za kusimikwa kwa Askofu huyo zilifanyikwa kwa
kuzingatia miongozo ya kanisa hilo ikiwemo kula kusoma hati mbalimbali za viapo
ili kulitumikia kanisa hilo.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa dini kutoka
dayosisi za Tanzania viongozi wa serikali wakiwemo wakuu wa wilaya pamoja
waumini wa dayosisi za Biharamulo na Kagera.
Mwisho
No comments:
Post a Comment