Mkuu wa wilaya ya Ngara Constantine Kanyasu |
DC Ngara atoa agizo kwa wazazi kuhusu Elimu
Na: Shaaban Ndyamukama –ngarakwetublogspot.com
Mkuu wa wilaya ya ngara mkoani Kagera Bw Costantine Kanyasu
amewataka wazazi kufanya maadalizi ya kuwaendeleza watoto wao kielimu mara
watakapochaguliwa baada ya kufaulu mitihani yao
Bw Kanyasu ametoa kauli hiyo alhamisi wiki hii katika mkutano
wake na wakazi wa kata ya Nyamiaga wilayani Ngara wakati wa mahafali ya 27 ya
darasa la saba katika shule ya msingi Kumuyange
Amesema wazazi wanalo jukumu la kuwalea watoto wao na
kuwaendeleza kielimu ili kukabiliana na ushindani wa ajira katika shirikisho la
afrika ya Mashariki kuliko kukaa nyumbani na kushindwa kazi za vibarua katika
shirikisho hilo
Amesema ni jambo la aibu kwa serikali ya Tanzania kuwa
vijana wasiojitambua kielimu na kuendelea kuwa maskini wakati nchi hii imejaa
rasilimali nyingi za kuweza kielimu
kutumika katika kuwekeza kwa kuwapeleka vijana kwenye shule mbalimbali
na kujifunza fani za kuwasaidia kimaisha
Amesema kuwa serikali imejipanga kuhakikisha wanafunzi
wanaochaguliwa kuingia sekondari au elimu ya juu wanakwenda na wazazi watakao kwamisha juhudi hizo vyombo
vya dola vitamchukulia hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kuwafungulia
mashtaka mahakamani
Picha ya dc
Katika hatua nyingine baadhi ya wadau wa elimu
katika wilaya ya Ngara mkoani
wamependekeza serikali kubadili utaratibu wa kutoa mitihani ya kuhitimu
elimu yamsingi kwa mfumo wa kuchagua
majibu yenye herufi sahihi kwa kuwa
mfumo huo unapoteza vipaji vya wanafunzi
kujieleza kwa kuandika .Meneja wa shule ya msigi na sekondari ya
RHEC wilaya ya Ngara ambaye
alikuwa ni mwenyekiti wa CCM wilayani
humo Bi Helena Adrian alisema mabadiliko
ya mara kwa mara katika mitaala ya elimu
nchini ni moja ya changamoto inayoikabili sekta ya elimu ambapo walimu
na wanafunzi wa shule za sekondari za serikali na watu binafsi kushindwa kutoa
taaluma inayokubalika na kuwa katika ushindani ndani ya afrika mashariki.
Alisema kuwa mitihani ya kuchagua imebainika kuwa na dosari kwa baadhi ya
wanafunzi kufaulu masomo kwenda ngazi nyingine
ya elimu wakiwa hawana taaluma inayokubalika na kuwapa wakati mugumu
walimu kufundisha mada ambazo hutumia muda mwingi kuzifanyia marudio katika
kufundisha wanafunzi wasiojua kusoma wala akuandika.
Naye Katibu wa mbunge
wa jimbo la Ngara mkoani Kagera kupitia CCM Bw Ruguge Nzutu Ruguge alisema kuwa kubadilika kwa mitaala kunawafanya
wanafunzi wa ngazi za elimu kutofautiana katika kufanya mitihani ikiwa ni
pamoja na lugha za kufanya mitihani hiyo kuhitilafina. Ruguge alisema kuwa wapo
wanafunzi wa shule binafsi kama Englis Medium kufanya masomo yao kwa lugha ya kiingereza na wengine wa
shule za msingi kutumia kiswahili katika kujifunza na kusababisha matabaka
katika utoaji wa elimu ndani ya kaya au katika jamii moja
Alisema kuna haja ya watunga sera za maendeleo ya taaluma
kubadili mfumo wa elimu ili kila mmoja apate elimu kwa kiwango kinachorandana
na mazingira yake kuliko kuiga sera za wageni na kuwa tegemezi katika taifa
hatimaye kuwa na wataalamu wasiojiweza kutafsri sheria na mikataba
Alidai serikali itoe tamkoa la lazima la kuwanusuru watoto wengine ambao hushindwa kupata elimu na kubaki mitaani wakiwa ombaomba na kukiuka
kauli mbiu ya mwalimu Nyerere ya kupata elimu kwa wote
Hawa ni
watoto wa mukibungere kata ya mabawe
wilayani Ngara ambao wamekosa haki yao ya kupata elimu
Katika tathmini ya elimu nchini kwa wadau hao mkuu wa wilaya ya Ngara Costantini Kanyasu aliwahimiza wahitimu wa ngazi za elimu wilayani humo kuwa waadilifu
katika jamii kwa kutumia elimu yao kufanya matendo yanayokubalika kisheria na
kuwa mfano bora kwa wale waliokwepa kwenda shule
Kanyasu alisema wazazi wanao wajibu mkubwa wa kutoa elimu kwa
watoto wao kwapatia elimu kwa kukwepa kulipia gharama za mafunzo kwa kuwa elimu
ni kuwekeza na ni mtaji wa familia endapo watakuwa karibu kufuatilia kile
mwanafunzi anachopata shuleni
‘’Kamawazazi mtawajibika na kulipa karo kwa wakati kisha
mkawa ni wafuatiliaji wazuri wa watoto wenu katika taaluma na wanafunzi kwa
namna yoyote wataweka bidii ya kujifunza
hatimaye kufanikiwa malengo yao na kuongeza uadilifu kwa
matendo yenye nidhamu.” Alisema Kanyasu
Alidai kuwa serikali
haina nafasi za ajira za kutosheleza maelfu ya wahitimu wa ngazi mbalimbali za
elimu kilichopo ni kujifunza fani zitakazowasaidia kujiajiri ili kujikwamua
kimaisha kwa kuanzisha ujasiliamali ulio na taaluma ndani yake kupambana na
umaskini katika familia na jamii kwa ujumla.
Aidha aliwataka wahitimu wa kidato cha nne kutumia elimu na maadili waliyopewa na walimu
wao kuandaa mazingira ya kuwa viongozi bora na watangulize uwajibikaji kwa
watakao pata ajira katika taasisi mbalimbali ndani na nje ya nchi.
No comments:
Post a Comment