Baadhi ya wakazi wa mji wa kabanga-Ngara wakiwa gulioni |
Na: Shaaban Ndyamukama Ngara
Wakazi wa
mji wa kata Kabanga
wilaya ya Ngara mkoani Kagera wameiomba halmashauri ya wilaya hiyo kuwapatia
uwanja maaluma kwa ajili ya soko na
kujenga chanja za kuuzia mazao yao
badala ya kuyauzia chini ya udongo
Wakiongea na
mwandishi wa habari hizi katika mji huo jana wananchi hao walisema kuwa wanafanya
biashara ya kuuza matunda na vyakula vibichi katika soko dogo karibu na mashamba ya watu na kushindwa
kuboresha biashara kwa wateja katika kuinua kipato
Mmoja wa
wakazi wa mji huo Sarafina Maulidi
alisema kuwa serikali haina budi kuandaa uwanja wa soko na wafanyabiashara
kujenga vibanda na chanja za kuwekea
bidhaa zao ikiwa ni pamoja na kujikinga na maradhi ya kipindupindu hasa wakati
wa mvua kali
Sarafina
alisema katika kupanga gulioni lisilotosheleza wakazi wa mji huo hulazimika
kulipa shilingi 100 kwa ajili ya kumlipa
mtu anayefanya usafi lakini fedha hizo ni nyingi kwa kila mwenye bidhaa na
vinywaji vya asili na zinapaswa kutumika
kwa ajili ya kuchimbia mashimo ya takataka pamoja na choo cha soko
Kwa upande wake Saidi Manywele alisema wananchi wanapata shida kwa kuwakiwa na jua kali ama kunyeshewa na
mvua hivyo panahitaji uboreshaji wa masoko wilayani Ngara
Alisema pia
licha ya serikali kupiga marufuku wakulima kuwatoza ushuru wa mazao
yapelekwayo gulioni kama viazi ndizi na mboga mboga bado watendaji wa
halmashauri ngazi ya kata wanaendelea kuwasumbua watu hao na kuwa kero ndani ya
jamii
Naye Kaimu
mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya ngara
Simon Mumbee alisema kwamba vipaumbele vya wananchi hupangwa na kamati
ya maendeleo ya kata WDC na kama watahamasishwa kupata soko la kisasa
halmashauri iko tayari kutekeleza matakwa yao
No comments:
Post a Comment