Askofu wa Jimbo Katoliki Rulenge-Ngara Severin Niwemugizi,akiwa na Dr peter Bujari Mkurugenzi wa HDT katika mahafali ya 30 kidato cha nne katika shule ya sekondari Mt. Alfred Rulenge |
Vijana tafuteni elimu
kwa kutanguliza dira katika maisha
Na,
Shaaban Ndyamukama –www.ngarakwetublogspot.com
Vijana wametakiwa kujiwekea
dira ya maisha katika kutafuta elimu ili kukabiliana na ushindani wa kupata
ajira duniani na kupambana na utandawazi kwa lengo la kudumisha maadili ya
kwenye jamii zao.
Mkurugenzi wa HDT mkoani Kagera
Dr peter Bujali ametoa kauli hiyo katika
mahafali ya 30 ya kidato cha nne kwa wanafunzi wa shule ya sekondari ya
Mt Alfred Rulenge(RAMA) iliyoko wilayani Ngara. Dr Bujari amesema kuwa vijana wengi wanashindwa kutimiza ndoto za maisha kwa kuwa hawana malengo wakati wakitafuta elimu na hatimaye kukosa
mwelekeo wa maisha yao
na kuendelea kuwa maskini
Amesema kuwa dira hizo
ziambatane na kuwajibika ipasavyo katika kutafuta taaluma kujenga uaminifu
katika utumishi nakukuza uchumi pamoja na kudai haki bila kuhatarisha amani. Aidha
Dr Bujali amesema mafanikio ya vijana yatapatikana endapo watafuata miiko na kulinda maadili ya jamii
kwa kufuata taratibu na sheria zilizowekwa na mamlaka iliyo juu yao
Alisema mataifa mengi
yamekumbwa na vurugu za kuvunjika kwa amani baada ya kukiuka taratibu na
maadili pale wanapopatikana watu wasiostahili nafasi zao kwa kutumia udini
ukabila na udugu unaopelekea kukiuka
haki wajibu na sheria
Alisisitiza vijana kuwa wanao
wajibu wa kutafuta taaluma kwa juhudi na maarifa ili kujikomboa na umaskini kwa
kushirikiana na wazazi au walezi wao wakiwemo walimu ili kuhakikisha wanafaulu
maisha wakiepuka tamaaza mahitaji wasiyo na uwezo nayo
No comments:
Post a Comment