Mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF wilayani Ngara Bw Ahmada abdallah |
Na Shaaban
Ndyamukama
Serikali imeshauriwa kurudisha elimu ya siasa katika shule
za msingi na sekondari pamoja na elimu
ya watu wazima ili kizazi kipya kiweze kutambua umuhimu wa demokrasia na haki
zao kisheria
Mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF wilayani Ngara Bw
Ahmada abdallah alitoa ushauri huo wakati akizungumza Ngara kwetu mjini Ngara akitoa maoni yake kuhusiana na maendeleo
ya jamii na demokrasia nchini hasa uhuru wa kuabudu kwa dini ya kikristo na kiislamu
Bw Abdallah alisema kuwa elimu ya siasa kwa shule za msingi
na sekondari pamoja na elimu ya watu wazima imebaki katika takwimu na wengi wanaoleta uvunjifu wa amani kidini
na katika sheria hawajapata elimu ya
uraia kwa kujua madhara na faida za kutumia demokrasia katika kudai haki zao.
Alisema serikali pamoja na viongozi wa dini hawana budi
kukaa na kujadili amani kwa waumini wao na kuweka mipaka katika kutoa maamuzi
bila kutumia vurugu na kuharibu mali za
wasiohusika na tukio
Alisema kwa kuwa serikali ya
Tanzania haina dini na inaongoza watu
wake wenye imani tofauti katika dini zao
ihakikishe inaweka mkazo wa sheria ili kulinda amani ya nchi inayotoa sifa kwa
taifa letu duniani Aidha alishauri halmashauri ya wilaya ya Ngara kushirikisha
wanasiasa katika kupanga na kuleta maendeleo ya
wananchi ili kuondoa changamoto zinazowakabili katika maeneo yao .“Viongozi
wa Vyama vya siasa ni wawakilishi wa wananchi na bila kufuata tofauti za
kisiasa wanao mchango wa mawazo kuhusu mahitaji ya wananchi yanayopaswa kuletwa
na serikali kupitia halmashauri husika” Alisema
Mwenyekiti huyo
Alidai kuwa kama miradi itakuwa wazi na kutolewa taarifa ya
mapato na matumizi kwa fedha za wananchi na zinazotolewa na serikali (Ruzuku)
haki itaonekana kupatikana na maendeleo yao.
No comments:
Post a Comment