Baadhi ya walimu wakipata semina elekezi ya usimamizi wa mitihani |
Na Shaaban
Ndyamukama Ngara
Wasimamizi
wa mtihani wa kuhitimu kidato cha nne katika wilaya ya Ngara mkoani Kagera
wametakiwa kufanya kazi waliyopewa kwa umakini na kutumia uadilifu kwa lengo la
kuleta ufaulu wenye sifa kwa wanafunzi watakaochaguliwa kuendelea na masomo ya
juu
Mkuu wa
wilaya ya Ngara Bw Costantini Kanyasu alisema hayo Oktoba 6 wilayani Ngara
katika ukumbi wa Ngara sekondari kwenye semina ya mafunzo elekezi kwa wasimamizi 135
walioteuliwa kusimamia mtihani wa kidato cha nne ulioanza oktoba 8 kote nchini
Kanyasu alisema
kuwa wasimamizi hao wajiepushe na udanganyifu wa mitihani wa kusaidia wanafuzi
wasiojiweza kitaaluma na hatimaye kupata wataalamu na watumishi wa kada mbalimbali
wasiojiweza katika kutoa huduma kwa taifa
Alimtaka
kila msimamizi kuwajibika kwa kufuata maelekezo na mwongozo wa baraza la
mitihani la taifa na kuandaa vijana watakao kuwa na manufaa ndani ya jamii kwa
kuzingatia kanuni taratibu na sheria
kuliko kuwa na vijana waliokwenda shule lakini wanakuwa wategemezi wa
taifa na kuendelea kuwa maskini kwa kukosa uadilifu
Naye Afisa
elimu sekondari wilayani Ngara Bw Julias Nestory alisema katika mtihani huo
wilaya ya Ngara itakuwa na watahiniwa 2471 kati yao 141 ni wale wa kujitegemea na
kutakuwa na vituo28 na kila chumba cha mtihani hakitazidisha wanafunzi 40.Nestory
alisema vijana wa kike baadhi yao wamejifungua na hawataruhusiwa kufanya
mtihani wa taifa wa kuhitimu elimu ya sekondari na wale wa kiume wamekimbia
familia zao kwa kukosa mahitaji muhimu ya elimu na kwenda kuwa vibarua katika
mikoa jirani kwenye mashamba ya miwa na
tumbaku. Alisema kuwa jamii haina budi
kuwamakini katika kuwekeza kwenye elimu kwani kati ya wanafunzi 2844 waliosajiliwa
kidato cha kwanza wilayani Ngara wanafuzi 543 hawatafanya mtihani huo kutokana
na sababu mbalimbali zikiweo za wazazi kushindwa kutoa mahitaji kwa watoto wao
Mara baada
ya kuanza mtihani huo siku ya jumatatu
oktoba 8 mwanafunzi wa shule ya sekondari Muyenzi wilayani Ngara Alexander
Victor miaka 18 aliugua ghafla katika shule hiyo baada ya kumaliza kipindi cha
kwanza cha somo la Civics
Kwa mujibu
wa mkuu wa shule ya sekondari Muyenzi Dickson Mwombeki (Mwenye koti Jeusi
Pichani ) alisema mwanafunzi huyo alipelekwa katika Hospitali ya Misheni
Rulenge kwa msaada wa gari la Afisa Elimu sekondari wilayani Ngara Juliu
Nestory Kilomita saba toka shuleni hapo
na kulazwa kabla ya kufanya somo la English. Akiongea na mwandishi wa habari
hizi mdogo wake na Mwanafunzi huyo Nelson Victor anayesoma kidato cha pili
shuleni hapo alisema kaka yake alikuwa mgonjwa siku tatu kabla ya mtihani
akisumbuliwa na homa kuumia miguu wakati wa kutembea pamoja kushindwa kula
Kwa upande
wake Mganga mkuu wa Hospitali ya Rulenge Dr Magnus Banyikila alisema mwanafunzi
Alexander aliugua ghafla kwa kupata maumivu ya mwili na kichwa na amepata
matibabu na kwa sasa ameruhusiwa kuendelea na masomo yanayofuata kwa mujibu wa
ratiba ya mtihani huo wa taifa
Afisa elimu
sekondari wilayani Ngara Juliu Nestory alithibitisha taarifa za kuugua
mwanafunzi huyo na kwamba kiafya amerudi katika hali yake ya kawaida na
kuungana na wenzake kufanya mtihani na somo ambalo hakulifanya taarifa za
daktari zitakuwa ni ushahidi kuondoa malalamiko
No comments:
Post a Comment