Kiongozi wa NCCR MAGEUZI ASIMAMISHWA
Na Mrisho Salum-NGARA
Chama cha NCCR-Mageuzi mkoani Kagera kimemsimamisha mwenyekiti
wa chama hicho wilayani Ngara Bw Kennedy Stanford Festo kwa kukiuka
katiba ya chama chake na kushiriki maadhimisho ya kuzaliwa kwa CCM
Kamishna
wa chama hicho mkoani Kagera Bw Peterson Mushenyera amesema kuwa uamuzi
huo umefikiwa katika kikao cha kamati tendaji ya chama hicho wilaya ya
Ngara kilichofanyika juzi
Amesema kuwa Bw Festo amesimamishwa kwa
muda wa siku 14 kutokana na kuvunja katiba ya chama chake na kuhudhuria
maadhimisho ya kuzaliwa kwa CCM yaliyofanyika February 5 katika kata ya
Kabanga wilayani Ngara
Bw Mushenyera amesema kuwa Bw Festo pia
ameandikiwa barua ya kujieleza kwa kamati ya nidhamu ya chama hicho
wilayani Ngara inayoongozwa na mwenyekiti Wyclif Samwel
Amenukuliwa
akisema Ninasema tunamsimamisha uenyekiti mpaka kesi yake itakapo
kwisha na chama chetu hakina ushirikiano na chama cha mapinduzi
Aidha
kamati hiyo ya utendaji ya NCCR-Mageuzi wilayani Ngara imemteua Bw
Joseph Bucha kukaimu nafasi ya mwenyekiti wa chama hicho wilayani Ngara
katika kipindi alichosimamishwa Bw Festo
No comments:
Post a Comment