February 9, 2015

KIBONDO SHOTOKAN KARATE CLUB (Kishoka)

Asalaam ayekhum mwana ngarakwetu blogu
Jumapili ya Februari 8 saa 12 kamili asubuhi nilikuwa katika DOJO la Kibondo. sehemu ambayo nimewahi kuwa mwanachama/mchezaji kwa miaka 3. Ilikuwa ni furaha sana kwangu,kukutana na wenzangu ambao kwa sasa ni zaidi ya mwaka mmoja tangu nimehama. Kikubwa zaidi ilikuwa kukuta Mtihani ukifanyika kwaajili ya kubadilisha Mikanda na kupanda madaraja. Sensei Onesmo Sylvanus anapewa pongezi kwakuuendeleza mchezo wa Karate wilayani Kibondo Mkoani Kagera.
Sensei One akimvalisha Mkanda wa Kijani(Green Belt) mmoja wa wanafunzi wake aliyekuwa na yellow Belt

Baadhi ya wachezaji wakishuhudia Sparling

Technics

Soft Sparling


Kutoka kulia ni Sensei One akiwa fuatiwa na Seniors Venance Mniga na Issa pamoja na wachezaji wengine

Sensei Onesmo Sylvanus
Niliondoka Kibondo saa 3 na dakika 26 asubuhi kurudi Biharamulo Mkoani Kagera. Lakini kwa bahati mbaya Pikipiki niliyokuwa nikisafiria ikapata Pancha kupelekea tube(Mpira wa ndani) gurudumu la nyuma kutoboka toboka. Hali hiyo ilinilazimu kuikokota hadi katika Kijiji cha kumkugwa maarufu kama Kilemba zaidi ya km 15 kutoka mjini. baada ya kuifungua nikaelekezwa na fundi kuwa haifai tena. Hivyo safari nhyingine ya Kurudi Kibondo Mjini kununua tube ikafanyika. Baada ya Kubadili tube safari ikaendelea. Nilifika Salama,namshukuru Mungu

Mafundi wakibadilisha tube

4 comments:

  1. Aksante sana kwa mjumuisho wa matukio yaliyo tokea katika dojo la hapo nyumbani, Ni wilaya ya Kibondo iliyokop Mokoani Kigoma ambako nilikuwa mwanafunzi tangu mwaka 2004 mpaka mwaka 2009 chini ya ufundishaji makini wa Sensei Onesmo akishirikiana na Sempai Mniga pamoja na Sempai Issa, kwakweli nakumbuka mbali sana nikiyaona mazingira ya nilikolelewa kwa upendo na umoja wa waalimu wangu, Pongezi pia ziwaendee waalimu wa Shule ya sekondari ya Malagarasi kwakuhakikisha tunajikwamua katika masuala ya kielimu.

    ReplyDelete
  2. Aksante sana kwa mjumuisho wa matukio yaliyo tokea katika dojo la hapo nyumbani, Ni wilaya ya Kibondo iliyokop Mokoani Kigoma ambako nilikuwa mwanafunzi tangu mwaka 2004 mpaka mwaka 2009 chini ya ufundishaji makini wa Sensei Onesmo akishirikiana na Sempai Mniga pamoja na Sempai Issa, kwakweli nakumbuka mbali sana nikiyaona mazingira ya nilikolelewa kwa upendo na umoja wa waalimu wangu, Pongezi pia ziwaendee waalimu wa Shule ya sekondari ya Malagarasi kwakuhakikisha tunajikwamua katika masuala ya kielimu.

    ReplyDelete
  3. Aksante sana kwa mjumuisho wa matukio yaliyo tokea katika dojo la hapo nyumbani, Ni wilaya ya Kibondo iliyokop Mokoani Kigoma ambako nilikuwa mwanafunzi tangu mwaka 2004 mpaka mwaka 2009 chini ya ufundishaji makini wa Sensei Onesmo akishirikiana na Sempai Mniga pamoja na Sempai Issa, kwakweli nakumbuka mbali sana nikiyaona mazingira ya nilikolelewa kwa upendo na umoja wa waalimu wangu, Pongezi pia ziwaendee waalimu wa Shule ya sekondari ya Malagarasi kwakuhakikisha tunajikwamua katika masuala ya kielimu.

    ReplyDelete