Makao Makuu ya Kanisa Katoliki
Duniani (Vatican) yamemsimamisha kazi Askofu wa Jimbo la Limburg, Ujerumani
Franz-Peter Tebartz-van Elst anayekabiliwa na kashfa ya matumizi mabaya ya
fedha kwa shughuli za kifahari.
Vatican ilieleza jana kuwa uamuzi
huo umechukuliwa baada ya kuridhika kuwa Askofu van Elst amekiuka maadili
yaliyowekwa na Papa Francis kwa viongozi walioko chini yake akiwataka waishi
maisha ya uchaji, umaskini.
Hadi sasa, kumekuwa na kelele nyingi
miongoni mwa waumini nchini Ujerumani wakitaka askofu huyo afukuzwe kazi.
Miongoni mwa matumizi yake makubwa
ni ujenzi wa makazi yake binafsi yaliyogharimu Euro 2.9 milioni (Dola 3.9
milioni), ukumbi wa chakula wenye mita za mraba 63 ambao ni pamoja na mesi na
bafu yenye thamani ya Euro 15,000.
Askofu van Elst (53) amekuwa
akituhumiwa kuendesha miradi hiyo kwenye mji wa kihistoria wa Limburg, ikiwamo
makumbusho, kumbi za mikutano, kanisa dogo na nyumba ya makazi yake binafsi.
Fedha hizo zinatokana na mapato
ambayo ni misamaha ya kodi kwa vikundi vya kidini nchini Ujerumani kwa mujibu
wa sheria.
“Baada ya uchunguzi wa awali,
Vatican imeamua kuchukua hatua kumsimamisha na kumwondoa kwenye usimamizi wa
jimbo,” ilieleza taarifa hiyo.
“Baba Mtakatifu (Francis) amekuwa
akifuatilia kwa karibu mambo yote yanayoendelea katika Jimbo la Limbuerg,”
iliongeza taarifa hiyo.
“Hali hiyo imefikia mahali ambako
kiongozi huyu hawezi kuendelea kusimamia kazi zake za kitume kama askofu wa
jimbo.”
Hata hivyo, taarifa hiyo haikueleza
ni kwa muda gani Askofu van Elst amesimamishwa kazi, ila iliongeza kuwa
itategemea na kukamilika kwa uchunguzi, tathmini ya hali ya fedha ya jimbo na
mambo mengine.
Wiki iliyopita, Askofu van Elst
alisafiri hadi mjini Rome, Italia kwa ndege ya shirika la gharama nafuu,
Ryanair kujieleza mbele ya Papa Francis – kutokana na madai kuwa alisafiri
mwaka jana kwa ndege ya daraja la kwanza kwenda India na pia kutumia vibaya
fedha
No comments:
Post a Comment