Mtu na mkewe wanagombana chumbani,
Ghafla ugomvi unakuwa mkubwa mke anaamua kukusanya vitu vyake
kwa lengo la kuondoka.
Mume anashangaa anamuuliza, Unakusanya vitu unaenda wapi?
Mke kwa nyodo anajibu, Nakwenda kwa mama yangu.
Mume naye akaanza kukusanya nguo zake na kuweka kwenye mabegi yake.
Mke kwa jeuri akamuuliza mume wake, Unapaki unakwenda wapi?
Mume akajibu kwa tabasamu, na mimi nakwenda kwa mama yangu.
Mke akauliza tena ''Hawa watoto wako watabaki na nani''?
Mume kwa kujiamini akajibu
'' Nao waende kwa mama yao kama sisi tunavyoenda kwa mama zetu''.
Mke alipigwa na bumbuwazi na baada ya akili kumkaa sawa wote wawili walikubaliana kurudisha virago vyao ndani na kutatua tofauti zao kwa njia ya kidiplomasia zaidi.
Ama kweli 'Dawa ya Moto ni Moto'.maoni:-tuma juveilla@gmail.com
maoni ya wadau
-
Juma Magoma Haaswaaa! hiyo ndo komoa nkukomoe,akimwaga mboga,mwaga ugali.
3 minutes ago via mobile ·
No comments:
Post a Comment