August 21, 2012
WANAUME WENGI NGARA WANA WANAWAKE ZAIDI YA MMOJA
Utafiti wa shirika lisilokuwa la kiserikali linalojihusha na utoaji wa elimu kwa familia, Global Family Enlightment Organization umebaini kuwa zaidi ya asilimia 88 ya wanaume walio katika ndoa mkoani Kagera wana wake wengine pembeni maarufu kama nyumba ndogo.
Mkurugenzi wa shirika hilo mkoani kagera Bw Inocent Bideberi amesema kuwa hali hiyo inarudisha nyuma maendeleo ya familia kwani wahusika wanashindwa kuhudumia familia zao
Bw Bideberi amesema utafiti umeonesha kuwa wanaume wangi wamekuwa na mwanamke zaidi ya mmoja.
Amesema shirika lake limeandaa mpango wa kuanza kutoa elimu kwa jamii ili kufahamu madhara ya kuwa na nyumba ndogo kwa familia.
Source: www.radiokwizera.com
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment