October 15, 2013

MTOTO ANUSURIKA KIFO KWA KULIPUKIWA NA BOMU-NGARA



MTOTO ANUSURIKA KUFA BAADA YA KULIPUKIWA NA BOMU -NGARA

Mtoto mmoja mkaziwa kijiji cha Mumiramila Kata kata ya Bugarama wilaya ya Ngara mkoani Kagera amenusurika kifo na baada ya kulipukiwa na bomu.

Mtoto huyo amejeruhiwa sehemumbalimbalizamwili wake na  amelazwa katika Hospitali ya misheni Rulenge wilayani humo kwaajili ya matibabu.

Mganga wazamu wa hospitali ya Rulenge Bi.Hilda Kagaruki amemtaja mtoto huyo kuwa ni Wema Kigenda (12) ambaye alijeruhiwa na bomu hilo lililomkata miguu miwili na kumtoboa tumbo nakupelekea utumbo wa ndani kutoka nje na kupoteza damu nyingi

Bi.Kagaruki amesema majeruhi huyo alifikishwa Hospitalini hapo Oktoba  11,2013 majira ya saa 11 jioni.

Akizungumza na Tanzania Daima,kaka wa mtoto aliyejeruhiwa aitwaye Sypriani Kigenda(18) amesema mdogo wake alilipukiwa na bomu hilo alipoliokota njiani wakati wakitokea shambani

“Mdogo wangu alikuwa nyuma yangu, nilishangaa kusikia mlipuko na kuona moto unawaka , niliporudi alipo nikakuta anavuja damu na michubuko miguuni na mwilini”Alisema

Hata hivyo Kaimu mganga mkuuwa Hospitaliya Rulenge Dk. Prosper Malya amesema kuwa jitihada za waganga na wauguzi kuokoa maisha ya mtoto huyo zinaendelea ambapo wamemuongezea damu na kushona majeraha

Jeshi la Polisi Mkoani Kagera limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba uchunguzi zaidi unaendelea.

Kamanda wa Polisi Mkoani humo Philip Kallangi ametoa wito kwa jamii kuepuka kuokota na kuchezea vitu visivyofahamika ambavyo vinaweza kusababisha madhara kama hayo.
majeruhi akiwa katika Hospitali ya Misheni rulenge alikolazwa

Sehemu ya miguu alipoumia

Akiongezewa damu.
Picha kwa hisani ya mwanablog wetu Shaaban Nassib Ndyamukama

No comments:

Post a Comment