Hadi jana mchana,
Miili ya watu 7 wanaosadikiwa kuwa
majambazi waliouawa kwa kupigwa risasi na askari wa jeshi la Polisi
wilayani Biharamulo Mkoa wa kagera iilikuwa
iukiendelea kuhifadhiwa katika Hospitali
teule ya wilaya hiyo baada ya ndugugu zao kukosekana
Kabla ya kifo chao, Watu hao 7
wakiwa na silaha za Kivita wameuawa kwa kupigwa risasi na askari wa jeshi la
Polisi wakati wakiwa katika msitu wa kijiji cha Mavota wakati wakijitayarisha
kuvamia na kufanya uharifu katika Mgodi wa dhahabu TULAWAKA wilayani Biharamulo
Mkoani Kagera march 10 mwaka huu
Akizungumza na Ngara kwetu Mganga
Mkuu wa Hospitali teule ya wilaya hiyo Dk. Gresmus Sebuyoya alisema Hospitali
yake inaendelea kuhifadhi miili hiyo kwakuwa ndugu wa marehemu hawajafika
kuitambua miili ya ndugu zao
Hata hivyo, Dk sebuyoya alisema
Hospitali hiyo inafanya mawasiliano na Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa
kagera Phillip Kallangi ili kupata Kibali cha kufanya mazishi ya miili
hiyo,kuepusha kuharibika vibaya na kutoa harufu kwakuwa iliharibiwa vibaya kwa
risasi
Tukio la majambazi hao kuuawa
limetokea March 10 mwaka huu na kuthibitishwa na Kamanda wa Jeshi la Polis Mkoani Kagera
Phillip Kalangi
Aidha Kamanda Kalangi amesema
kufanikisha udhibiti wa uharifu na kuuawa kwa majambazi hao,kumetokana na
taarifa ziliripotiwa na wananchi kwa jeshi la Polis.
Nafurahia kupata hii blog!Nilikuwa najaribu kuangalia kama kuna kitu kama hii blog,basi leo nimefurahi kuiona.Asante kwa kutujulisha habari za huko sie tulioko nje ya Ngara.Kila jema na endelea kutujuza mambo ya huko hasa mikakati ya maendeleo mfano,mikutano ya vijiji,Kata,Tarafa,Wilaya na jinsi wanavyopanga maendeleo.
ReplyDelete