December 11, 2012

DC-KIBONDO ATOA SHILINGI LAKII 8 KWA KANISA LA SABATO


Kutoka Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Kibondo-Kigoma akiwa na Hundi ya shilingi laki nane aliyoikabidhi kwa Kanisa la Adventist SABATO, anayefuata ni Mwl Clavery Ntindyicha Katibu wa  Kamati ya amani na maridhiano lkn pi mwenyekiti wa CHADEMA Wilayani humo. na kulia ni Kiongozi wa kanisa la SABATO na afisa mahusiano na Habari katika Kanisa hilo William Ndyana. Picha imepigwa katika Ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Kibondo

Kulia katika Picha ni Kiongozi wa Kanisa la SABATO na afisa mahusiano na Habari katika Kanisa hilo William Ndyana akimkabidhi CD yenye Matukio mbali mbali ya Ufunguzi na ufungaji wa Makambi katika kanisa hilo akiikabidhi kwa Katibu wa kamati ya amani na Maridhiano Mwl Clavery Ntidyicha ili nae akikabidhi kwa Mkuu wa Wilaya Kibondo Venance mwamoto.

Kushoto ni DC Mwamoto akipokea CD ya kanisa la SABATO kutoka kwa Mwl Clavery Ntidyicha

Hiyo ndio Cheque yenye thamani ya Shilingi Laki 8,ambayo DC Mwamoto ameikabidhi kwa kanisa la SABATO Kanyamahela Kibondo

Kiongozi wa kanisa la SABATO na afisa mahusiano na Habari katika Kanisa hilo William Ndyana kulia akipokea Cheque iliyotolewa na Mkuu wa wilaya ya Kibondo Venance Mwamoto. anayeonekana katika Picha ni Mwl Clavery Ntidyicha aliyepewa jukumu na DC kukabidhi hundi hiyo
ABaada ya shughuli hiyo, nami kama Mwanahabari nikapewa CD hiyo



KIBONDO
Mkuu wa wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma Bw. Venance Mwamoto amelikabidhi kanisa la Adventist Sabato kanyamahela wilayani humo Hundi yenye thamani ya Shilingi Laki nane kwaajili ya maendeleo ya Vijana wa Kanisa hilo

Bw. Mwamoto amekabidhi hundi hiyo kwa Kiongozi wa mahusiano na habari wa kanisa hilo Bw. William Ndyana katika Ofis ya mkuu huyo wa wilaya
Mkuu huyo wa wilaya amesema hndii hiyo inatokana na ahadi yake aliyoitoa wakati alipoalikwa kuwa mgeni rasmi katika kufunga shughuli za makambi ya vijana wanaojifunza Saikolojia katika Kanisa hilo na kwamba fedha hiyo ni kwaajili ya sare na ujenzi wa kanisa

Baada ya kukabidhiwa hundi hiyo,Kiongozi wa kanisa Bw. William Ndyana amesema watahakikisha fedha hiyo inatumika katika makusudio husika na kuyataka mashirika mengine kuiga mfano wa mkuu huyo wa wilaya katika kusaidia Taasisi kama makanisa kwaajili ya shughuli za maendeleo.    

No comments:

Post a Comment