Makundi ya wanaharakati nchini
huenda wakakutana na Rais Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar Es Salaam kati ya kesho
au keshokutwa, kwa ajili ya mazungumzo kuhusu Muswada wa Marekebisho ya Sheria
ya Mabadiliko ya Katiba
Hatua hiyo inakuja baada ya Rais
Kikwete kukutana na kundi la viongozi wa vyama vya siasa vyenye uwakilishi
Bungeni na kujadili mambo mbalimbali kuhusu marekebisho ya Muswada huo.
Rais Kikwete leo amekutana na
viongozi wa CUF, Chadema na NCCR-Mageuzi na kujadiliana kasoro kadhaa zilizopo kwenye
Muswada huo uliozua utata na kusababisha vyama hivyo kuitisha maandamano ya
nchi nzima kupinga musawada huo usisainiwe na rais kabla ya kuyasitisha
maandamano hayo
Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba nchini
(Jukata) Bw Deus Kibamba, amesema kuwa wameahidiwa kuwa wanaweza kuonana na
Rais kati ya Jumatano au Alhamisi kwa ajili ya kujadili Muswada huo
No comments:
Post a Comment