Taarifa za kifo cha Nelson Mzee Nelson Mandela zimetolewa
na Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma
Rais Zuma amesema kuwa mzee Mandela amefariki
akiwa na miaka 95.
Rais wa nchi hiyo Jacob Zuma amesema taifa
limepoteza baba wa taifa na bendera zitapepea nusu mlingoti kufuatia msiba huo
mkubwa kwa taifa hilo.Mandela amekuwa
akiugua kwa muda mrefu.
Naye rais wa Marekani Barack Obama amesema nchi ya Afrika Kusini pamoja na dunia kwa ujumla imepoteza mtu muhimu
Naye rais wa Marekani Barack Obama amesema nchi ya Afrika Kusini pamoja na dunia kwa ujumla imepoteza mtu muhimu
Maisha yake
Nelson Rolihlahla
Mandela alikuwa mwanasiasa mkongwe na mwanaharakati aliyepambana na sera za
ubaguzi za makaburu wa Afrika Kusini na hatimaye kuwa Rais wa kwanza Mwafrika
nchini humo. Ni mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel. Mbali na tuzo hiyo,
ameshatunukiwa zaidi ya tuzo 250 katika miongo minne iliyopita.
Alizaliwa Julai 18
mwaka 1918. Ni rais wa kwanza aliyechaguliwa kidemokrasia nchini Afrika Kusini.
Alikuwa mwanasheria na mwanachama wa Chama cha African National Congress (ANC)
aliyepinga siasa ya ubaguzi nchini Afrika Kusini.
Mandela anatokea
katika ukoo wa Thembu uliokuwa ukitawala mkoa wa Transkei lililopo katika jimbo
la Eastern Cape. Alizaliwa katika Kijiji cha
Mvezo katika Wilaya ya Umtata na ana asili ya Kabila la Khoisan kwa upande
wa mama yake.
Babu yake wa upande wa
mama aliyefariki mwaka 1832 Ngubengcuka, alikuwa mfalme wa ukoo wa Thembu
na mmoja kati ya watoto wake aliitwa Mandela. Huyo ndiyo Babu yake Nelson na
chanzo cha jina hilo la ukoo.
Baba yake Mandela Gadla
Henry Mphakanyiswa alikuwa chifu wa mji wa Mvezo, hata hivyo baadaye
aliondolewa na wakoloni katika cheo hicho na kubaki kuwa mjumbe wa baraza.
Mphakanyiswa alikuwa na wake wanne ambao walimpatia watoto 13, wanaume wanne na
wanawake tisa.
Mandela alizaliwa kwa mke
wa tatu na kupewa jina la Rolihlahla likiwa na maana ya kuvuta tawi la mti au
kwa nahau ‘msababisha matatizo’.
Rolihlahla alikuwa
mtoto wa kwanza katika familia yao kwenda shule ambako mwalimu wake Mdingane
alimpa jina la Nelson. Baba yake alifariki kwa ugonjwa wa kifua kikuu wakati
Mandela akiwa na umri wa miaka tisa, hivyo ndugu yake aitwaye Jongintaba akawa
mlezi wake.
Alisomea katika Shule
ya Misheni ya Wesleyan. Alipofikisha miaka 16 alijiunga na Taasisi ya
Clarkebury kwa miaka miwili ambapo alipata cheti cha awali. Mwaka 1937 alihamia
katika mji wa Healdtown katika chuo kingine cha Wesleyan. Akiwa na miaka 19
alijihusisha na michezo ya masumbwi na riadha.
Baadaye alijiunga na
Chuo Kikuu cha Fort Hare, ambapo alichukua shahada ya Sanaa na
hapo ndipo alipokutana na Oliver Tambo ambaye aliendelea kuwa rafiki yake kwa
muda mrefu.
Baada ya mwisho wa
mwaka wa kwanza, Mandela alijihusisha na mgomo ulioandaliwa na baraza la
wanafunzi wakipinga sera za chuo hicho. Matokeo yake alifukuzwa shule hadi pale
atakapokubali masharti ya chuo. Baadaye akiwa jela, Mandela alisoma shahada ya
sheria kutoka Chuo Kikuu cha London katika programu ya nje.
Baada ya kufukuzwa
shule, mlezi wake Jongintaba alimtaka aoe akiwa na ndugu yake Justice. Hata
hivyo, Mandela hakutaka na hivyo akakimbilia mjini Johannesburg ambako alitafuta kazi ya ulinzi kwenye migodi ya madini, kazi
ambayo hakuifanya kwa muda mrefu.
Baadaye Mandela
alianza kufanya kazi ya usaidizi wa ofisi katika ofisi ya sheria mjini
Johanesburg. Akiwa hapo alikamilisha masomo yake ya Shahada ya Sanaa katika
Chuo Kikuu cha Afrika Kusini kwa njia ya posta na baada ya hapo alianza masomo
ya sheria katika Chuo Kikuu cha Witwatersrand
ambako alikutana na marafiki wengine waliopambana katika vita ya ubaguzi wa
rangi ambao ni Joe Slovo, Harry Schwarz na Ruth First.
Siasa
www.ngarakwetu.blogspot.com
Baada ya ushindi wa
chama cha Afrikaner wa mwaka 1948 kilichokuwa kikiunga mkono ubaguzi wa rangi,
Mandela alianza kujihusisha rasmi na siasa. Alikiongoza chama cha ANC katika
kampeni za uasi za mwaka 1952 na mkutano wa mwaka 1955 ambao ulizaa mchakato wa
uhuru na kuweka msingi wa kupiga ubaguzi wa rangi.
Akiwa amevutiwa na
siasa za aliyekuwa Waziri Mkuu wa Indiawakati huo Mahatma Gandhi, Mandela alianza kufanya upinzani
usio na vurugu.
Mwaka 1956, alikamatwa
akiwa na wafuasi wake 150 na kushitakiwa kwa uhaini. Hata hivyo baada ya kesi
hiyo kwenda hadi mwaka 1961, waliachiwa huru.
Kifungo cha maisha
Mwaka huohuo 1961
Mandela aliteuliwa kuwa kiongozi wa kikosi cha silaha kikijulikana kama ‘Umkhoto we Sizwe’. Aliratibu mapambano dhidi ya majeshi ya
Serikali na kuweka mikakati ya vita vya msituni, kama hujuma za kukomesha
ubaguzi zingekwama.
Agosti 5, 1962 Mandela
alikamatwa na majeshi ya Serikali na kuwekwa jela ya Johannesburg baada ya kupotea kwa miezi 17.
Makundi mbalimbali
yalihusishwa na njama za kukamatwa kwake kikiwemo Chama cha South African
Communist Party na kitengo cha Intelijensia cha Marekani (CIA). Hata hivyo
Mandela hakutilia maanani madai hayo.
Juni 12, 1964, Mandela
alihukumiwa kifungo cha maisha baada ya kujitetea mahakamani kuhusu harakati zake
dhidi ya ubaguzi wa rangi. Alipelekwa katika gereza lililopo katika Kisiwa cha
Robben.
Februari 2, 1990
aliyekuwa rais wa Afrika Kusini Fredrick de Klerk aliondoa amri ya kukipiga
marufuku chama cha ANC na makundi mengine yanayopinga ubaguzi wa rangi na
akatangaza kumwachia huru Mandela. Aliachiwa rasmi Februari 11, 1990
tukio lililoonyeshwa dunia nzima.
Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya marehemu.Amina! www.ngarakwetu.blogspot.com
No comments:
Post a Comment