March 18, 2014

Jaji Warioba awapa raha watanzania.Apigilia msumari serikali 3


MWENYEKITI wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, amezima rasmi sakata la makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kulazimisha Bunge Maalumu la Katiba kukataa pendekezo la Tume ya Mabadiliko ya Katiba kuhusu muundo wa Muungano wa serikali tatu.
Akiwasilisha Rasimu ya Pili ya Katiba bungeni jana, Jaji Warioba alisema uchambuzi uliofanywa na tume yake umezingatia maoni ya wananchi, historia  na hali halisi, na kwamba ili muungano udumu serikali tatu hazikwepeki.
Alisema tume ilitafakari maoni mbalimbali yaliyotolewa na wananachi na makundi, na ilirejea ripoti kadhaa za miaka zaidi ya 20 mfululizo, ikazingatia malalamiko ya Zanzibar na Tanganyika, mgongano wa kikatiba kati ya Katiba ya Zanzibar na ya Muungano, na mengine mengi

No comments:

Post a Comment