MULEBA:
Madiwani na viongozi wa CCM
wilayani Muleba mkoani kagera wametakiwa
kuacha malumbano ya kisiasa na badala yake
yake wahimize upatikanaji wa maendeleo kwa wananchi
Waziri wa Ardhi na maendeleo
ya makazi Profesa Anna Tibaijuka ametoa kauli hiyo jana kwenye kikao cha
madiwani wa ccm na viongozi wa chama hicho
katika kuondoa migogoro iliyopo kwa viongozi hao wilayani humo
Profesa Tibaikuka maesema
kuwa vitendo vya kulumbana na kuendeleza migogoro ni kukiweka chama katika
mazingira magumu katika uchaguzi ujao na wanachi kushindwa kuamini wakiwemo viongozi
waliowachagua
Prof Tibaijuka akisaini kitabu cha wageni,pembeni yake ni m/kiti wa CCM wilayani Muleba Muhaji Bushako |
Profesa Anna Tibaijuka akisaini kitabu katika kufanya
mkutano na viongozi wa ccm wilayani Mulena kulia ni Mwenyekiti wa CCM wilayani
Muleba Muhaji Bushako
Hata hivyo Mwenye kiti wa CCM
wilayani Muleba Bw Muhaji Bushako amesema malumbano yalisababishwa na ukiukaji
wa misingi ya uongozi na katiba ya chama lakini
sasa kuna maridhiano na migogoro sasa imekwisha.
Vijana washauriwa kuwa
wajasiliamali
Na Shaaban Ndyamukama
November 12, 2013
MULEBA
Waziri wa ardhi na maendeleo
ya makazi profesa Anna Tibaijuka amelitaka kundi la Vijana kujiunga katika
vikundi vya uzalishaji mali
na kufanya kazi kwa juhudi na maarifa ili kujiletea maendeleo kwenye maeneo yao
Profesa Tibaijuka ametoa wito
huo jana katika ziara yake ya kutembelea wnanchi wa kijiji cha kisana wilayani
Muleba katika kukagua miradi ya maendeleo na kwamba vikundi vyenye miradi
ataviwezesha kiujasiliamali
Amesema kundi la vijana lina
maisha ya kutegemea ajiraa kutoka serikalini lakini fursa hiyo inapatikana kw
watu wachache tena wenye taaluma ambao
ni katika nyanja za elimu afya na miundombinu
Hata hivyo Profesa Tibaijuka
jana ametoa Jumla ya shilingi milioni 1.3 kwa ajili ya kuwezesha vikundi vya
ujasiliamali vya kata ya Kyebitembe kikiwemo cha vijana cha kutokomeza ugonjwa wa
mnyauko wa migomba.
Wananchi waomba kuongezewa
nguvu za ujenzi wa zahanati ya kijiji
Na Shaaban Ndyamukama
November 12, 2013
MULEBA
Wananchi wa kijiji cha kisana
wilayani Mulea mkoani Kagera wamejenga zahanati yao
ya kijiji kwa kukusanya vifaa
vinavyopatikana katika maingira yao
ambavyo thamani yake ni shilingi milioni 17.8 bila nguvu za serikali
Diwani wa kata ya Kyebitembe
wilayani Muleba Bw Vedasto Rwechungura amesema hayo jana wakati akitoa taarifa
ya maendeleo kwa waziri wa ardhi na
mendeleo ya makazi Profesa Anna Tibaijuka
Bw Rwechungura amesema
zahanati hiyo jengolake limefikia hatua ya kufunga linta ambapo kijji hicho kilijenga
baada ya kutenga maeneo ya huduma za jamii katika matumizi bora ya ardhi
Waziri Tibaijuka akikagua jengo
la zahanati la kijiji cha kisana wilayani Muleba linalojengwa kwa Nguvu za
wananchi jinsi linavyoonekana ,mwenye skafu ni diwani kata ya Kyebtembe
Vedastus Rwechungura
Mkurugenzi mtendaji wa H/w ya MulebaBi Oliva Vavunge akifafanua kuhusu ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Kisana |
Hata vivyo Mkurugenzi wa
Halmashauri ya wilaya ya Muleba Bi Oliva Vavunge amesema mwaka huu zimetengwa
shilingi milioni 60 kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa zahanati hiyo ili kuwapa
nguvu wananchi kujitolea.
WORLD VISSION yasaidia
jamii Kujenga vyumba vya madarasa
Na Shaaban Ndyamukama
MULEBA
Shirika la world vision kanda ya kagera jana limekabidhi
vyumba vitatu vya madarasa katika shule ya msingi Nyailigamba wilayani Muleba
mkoni Kagera vilivyojengwa kwa Tsh.mil 36.7 zikiwemo Nguvu za wananchi
Diwani wa kata ya Muhutwe Magongo Justus amesema ujenzi huo
umefanyika kunusuru wanafunzi 400 wa shule hiyo kujifunzia mazingira magumu
ikiwa nguvu za jamii ni Tsh.mil 2.4 na mbunge wa Muleba kaskazini amechangia
matofali 30,000
Justus amesema kuwa halmashauri ya wilaya ya Muleba
imechangia Tsh Mil 6 na mkuu wa wilaya hiyo Lambris Kipuyo alichangia Tsh
600,000/- na kwamba vyumba hivyo
vitatumika kwa alengo yaliyokusudiwa
Hata hivyo Meneja wa world vision Kanda ya kagera Misigaro
Mpiti amesema shirika lake
linasaidia jamii
changamoto zilizoibuliwa na kupewa kipaumbele katika kuhitaji misaada
No comments:
Post a Comment