January 14, 2016

BARAZA LA MADIWANI HALMASHAURI YA MJI KAHAMA

Kutoka Kulia ni Mbunge wa jimbo la kahama Bw.Jumanne kishimba,Bi.Salome Makamba Mbunge wa Viti Maalum CHADEMA-Shinyanga,Mkurugenzi mtendaji halmashauri ya Mji Kahama Bw.Anderson Musumba,Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Abel Shija na Makamu wake Mary Manyambu wakati wa kuimba wimbo wa Taifa Kabla ya kuanza kwa kikao cha barza la Madiwani. picha na Juventus Juvenary

Baahi ya wakuu wa idara Kutoka kulia ni Bi. Anastazia Manumbu Idara ya elimu sekondari,Katikati ni Aliko Luko Idara ya elimu Shule za msingi na kushoto ni Afisa utumishi Bw.Stephen Kulwa

Mbunge wa Viti Maalum CHADEMA-Mkoa wa Shinyanga Bi.Salome Makamba

Baadhi ya Madiwani wakifuatilia na kusikiliza hoja na Michango ya wenzao

Kushoto,ni Mwanahabari Mohab Dominick anayeandikia Gazeti la Nipashe (IPP) akitekeleza wajibu wake

MEZA KUU

Madiwani wakiendelea na kikao


KAHAMA

Wakuu wa idara wilayani Kahama Mkoani Shinyanga wametakiwa kujenga tabia za kuwatembelea madiwani na kukusanya taarifa za maendeleo ya Miradi inayojengwa kama sehemu ya uwajibikaji

Rai hiyo imetolewa na Mbunge wa jimbo la kahama Bw. Jumanne Kishimba wakati akitoa Mchango kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa halmashauri ya Mji huo

Bw. Kishimba amesema kuna baadhi ya wakuu wa Idara ambao wamekuwa wakiratibu  na kuandaa taarifa za ujenzi wa Miradi hiyo wakiwa Ofisini bila kuwashirikisha madiwani
Mbunge huyo amesema jambo hilo siyo sahihi kwakuwa madiwani ndio wawakilishi wa wananchi hivyo wanatakiwa kuhusishwa katika kuandaa na kutoa taarifa hizo

No comments:

Post a Comment