May 20, 2016

MAGUFULI AMTUMBUA KITWANGA


1 comment:

  1. JJ

    Saturday,May 21, 2016

    KAHAMA
    Baadhi ya wananchi wa Mji wa kahama Mkoani Shinyanga wamekuwa na maoni tofauti kuhusu maamuzi ya Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli kutengua uteuzi wa Waziri wa Mambo ya Ndani Charles Kitwanga huku baadhi wakieleza kuwa tukio hilo litaimarisha nidhamu kwa viongozi wa umma

    Wananchi hao wametoa maoni hayo kufuatia Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Ikulu kuwa,Rais amemsimamisha kazi waziri huyo baada ya kubainika kuwa ameingia Bungeni na kujibu swali linalohusu wizara yake huku akiwa amelewa pombe

    Mmoja wa wananchi hao Bw.John Bundala amesema kuwa Nidhamu kwa watumishi wa umma ni jambo muhimu hivyo adhabu iliyotolewa kwa waziri wa mambo ya ndani ni fundisho kwa wengine

    Kwa upande wake Bi.Magreth Ndalo amesema watumishi wa umma hawanabudi kuwa na nidhamu sasamba na viongozi wa kuchaguliwa,hivyo kitendo kilichotekelezwa na rais ni sehemu ya uwajibikaji kwaajili ya kuimarisha utawala bora.

    ReplyDelete