MKUU wa Wilaya ya Ngara, Constantine Kanyasu, amewashauri wananchi wa wilaya hiyo kutoa ushirikiano wakati wa zoezi la Sensa ya Watu na Makazi linalotarajiwa kufanyika Agosti 26 mwaka huu.
Akizungumza na Tanzania Daima jana mjini hapa, Kanyasu, alisema wananchi wana wajibu wa kutoa taarifa zao sahihi, ili kuiwezesha serikali kupanga na kuweka mikakati mbalimbali ya maendeleo kwa kuzingatia idadi ya wakazi waliopo nchini.
Alisema serikali yoyote duniani, haiwezi kuweka mikakati madhubuti ya maendeleo kwa wananchi wake bila kujua idadi kamili ya watu wake na kuongeza kuwa taarifa zote zitakazotolewa zitakuwa ni siri.
Akizungumzia changamoto zilizopo katika wilaya hiyo iliyoko mpakani mwa nchi za Burundi na Rwanda kutokana na mwingiliano wa watu tofauti, alisema wilaya yake imejipanga kikamilifu ili kufanikisha zoezi la sensa.
Alisema Wilaya ya Ngara itahakikisha kila mtu aliyelala katika wilaya hiyo atahesabiwa, ili kukamilisha azima ya serikali katika zoezi
------------Tanzania Daima.............. |
No comments:
Post a Comment