Na Shaaban Ndyamukama Ngara
Hospitali tatu na vituo vitatu vya Afya katika wilaya ya
Ngara mkoani Kagera zimepata msaada wa mshuka
380 kutoka Mfuko wa Bima ya Afya NHIF nchini kama moja ya hamasa kwa
wagonjwa kuchangia mfuko huo na jamii kupata huduma za afya bila kutumia
gharama kubwa za matibabu
Mbunge wa jimbo la ngara mkoani kagera Bw Deogratias
Ntukamazina alitoa mashuka hayo hivi
karibuni wilayani Ngara katika hospitali
za Nyamiaga inayoendeshwa na serikali
kwa kuipatia mashuka 100 na mbili za binafsi za Murugwanza inayomilikiwa
na kanisa Anglican mashuka 100 pamoja na
Hospitali ya Rulenge inayomilikiwa na kanisa katoliki jimboni humo nayo ilipata
shuka 100
Bw Ntukamazina ambaye ni mwenyekiti wa bima ya afya Taifa
alisema mashuka hayo ni katika
kuhamasisha jamii kuchangia na kutumia huduma ya bima ya afya kila kaya kwa
kupunguza gharama za matibabu ambazo ni kubwa kuzimudu mtu mmoja kila kaya moja
au kwa mtu binafsi kutokana na dawa kuwa pungufu katika Hospitali na zahanati
Aidha vituo vya Afya vya Bukiriro Mabawe na Murusagamba
vilipata msaada wa mashuka 20 kila kimoja kusaidia wagonjwa wanaolazwa katika
vituo hivyo katika harakati za kupata matibabu na ambao wengi wao ni watoto
chini ya miaka mitano na akina mama wajawazito
Katika hatua nyingine mbunge huyo alitoa majaketi yanayoakisi
mwanga nyakati za usiku kwa baadhi ya waendesha pikipiki katika wilaya ya ngara
mkoani kagera ili kujikinga na ajali zisizo za lazima
Waendesha pikipiki walionufaika na msaada huo ni kutoka vituo vya Rulenge Ngara mjini na
Nyakisasa ambapo mbunge alisema kuwa
vijana wa maeneo hayo huzunguka maeneo mengi wilayani humo na baadhi kupata ajali na kuhatarisha maisha
yao
Alisema kuwa vijana hao wapatao 150 waliopata majaketi hayo
kutoka NHIF watakuwa kichocheo cha
uhamasishaji wananchi kuchangia bima ya afya kwa kutoa shilingi 10000/= kila
kaya kwa mfuko wa CHF na kutibiwa bure katika kadi ya watu watano.
No comments:
Post a Comment